Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.

Maelezo ya Jumla

Historia yetu

Historia ya Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaani mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya Biashara, iligawanywa katika tanzu tatu tofauti:

 • NBC Holding Corporation
 • National Microfinance Bank (NMB)
 • NBC (1997) Limited

Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), lilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.

Mambo ya Kujivunia

 • Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini
 • Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha na huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali
 • Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima

Tuzo na zawadi zetu

 1. 2005: Bankers Awards (Corporate Bank of the Year)
 2. 2005: Bankers Awards (Special Technology Awards)
 3. 2009: TRA Compliant Large Tax Payer Award
 4. 2009: African Banker Award (Best Local Bank in Africa)
 5. 2015: Asian Banker Award (Best Retail Bank)
 6. 2015: NBC Voted 2015 – 16 Superbrands
 7. 2017: Best Islamic Retail Bank Award
 8. 2017: NBC Voted 2017 – 18 Superbrands
 9. 2018: 1st in the Financial Category and 2nd Overall winner – 42nd Dar es Salaam International Trade Fair
 10. 2018: 1st in the Financial Category and 2nd Overall winner – 1st National Farmers Day
 11. 2018: 1st in the Financial Category and 2nd Overall winner – 1st National Mining Technology and Investment Exhibition

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 (0) 768 984 000 | +255 (0) 222 193 000 | +255 (0) 225 511 000 | 0800711177 (Toll-Free)

Tuandikie baruapepe:

 NBC_MarketingDepartment@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC