Akaunti Binafsi ya Hundi ya NBC inakupa njia rahisi na nzuri inayokusaidia kudhibiti matumizi ya fedha yako. Kwa kuongezea, unao uhuru wa kuweka na kuchukua fedha kwenye Akaunti yako kama upendavyo

Fungua Akaunti

Faida za kuwa na Akaunti Binafsi ya Hundi ya NBC

Ultimate account - card image
Hand holding plus sign icon
Kufungua akaunti

Jaza fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi la NBC lililo karibu nawe.

Nyaraka zifuatazo zitahitajika:

 • Picha ndogo mbili za rangi zilizopigwa siku za karibuni
 • Kitambulisho chako – mojawapo ya hivi vifuatavyo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura
 • Uthibitisho wa anuani ya makazi – mojawapo ya nyaraka zifuatazo:
  • Risiti ya malipo ya bili ya maji au umeme (iliyolipwa ndani ya miezi sita) inayoonesha anuani ya makazi yako
  • Barua rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali ya mtaa
  • Barua ya mwanasheria ikiainisha wazi makazi yako
 • Kwa wasio raia wa Tanzania watahitajika kuleta:- pasi ya kusafiria, kibali cha kazi au cha makazi
Information - icon
Akaunti Binafsi ya NBC inakuwezesha
 • Kuweka na kuchukua fedha kwenye akaunti yako bila mipaka yoyote
 • Kadi ya benki (NBC Visa debit card) BURE unapoanza
 • Unapata huduma za Kibenki kwa njia ya mtandao,  kwa njia ya simu ya mkononi na kupitia kwa mawakala wa NBC
Checklist - icon
Taarifa muhimu
 • Akaunti Binafsi ya NBC ni kwa fedha za Kitanzania tu

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC