Ukiwa na Huduma za NBC Mobile Banking, una benki mfukoni kwako. Unatakiwa tu kuwa na simu yako ya mkononi, unaweza kutekeleza miamala mingi ya kibenki popote, wakati wowote.

Namna inavyofanya kazi

mobile device - icon
Get started

Enjoy banking at your fingertips – download our app now.

confirm - icon
Kulipa bili kwa watoa huduma wengi zaidi
  • Kuangalia salio na kupata taarifa fupi ya akaunti yako
  • Kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti zako nyingine zilizoungaishwa na akaunti yako na kwenda kwenye akaunti nyingine za NBC
  • Kutuma fedha kwenye mitandao ya simu ya mkononi (MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, na EZYPESA)
  • Kununua muda wa maongezi kwa ajili ya namba yako yoyote ya simu ya mkononi
  • Kutunza namba za akaunti au simu kwa wale unaowatumia hela au zile unazozitumia kulipa bili za mara kwa mara
  • Badili Namba yako ya Siri mara nyingi kadiri inavyowezekana
  • Kuchagua lugha unayoipendelea zaidi
mobile device - icon
Unajisajilije kwenye Huduma za Kibenki kwa Njia ya Simu ya Mkononi?
  •  Jaza Fomu hii kisha ipeleke kwenye tawi lolote la NBC lililo karibu yako ili kukamilisha usajilu.  Kujisajili ni bure
  • Utapokea ujumbe mfupi kwenye simu yako ya mkononi punde tu utakapokuwa umeunganishwa huduma NBC Mobile Banking iitakapokuwa tayari imeunganishwa
  • Piga tu *150*55#  kisha fuata maelekezo rahisi
mobile device - icon
Ni salama kiasi gani?

Usalama umehakikishwa kwenye huduma za kibenki za NBC kwa njia ya simu ya mkononi. Miamala yote kwenye simu ya mkononi itahitaji Namba yako ya Siri na Namba yako ya Siri itahitajika kila mara unapohitaji huduma hizi. Ni wajibu wako kutunza kwa usiri mkubwa Namba yako ya Siri ili kuepuka miamala isiyo halali kufanyika.

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC