Ikiwa wewe unataka kununua nyumba kwa mara ya kwanza au kununua nyumba nyingine, Mkopo wa Kununua Nyumba wa NBC utakusaidia kufanya hayo yote–kwa gharama nafuu na huduma za ushauri wa kitaalam

  Ninahitaji Mkopo

Ninapataje Mkopo wa Kununua Nyumba?

Namna ya Kuomba Mkopo wa Kununua Nyumba

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi la NBC lililopo karibu nawe.

Vitu vya kuwa navyo unapoomba mkopo huu

 • Nakala ya Kitambulisho kimoja kati ya vifuatavyo:-  Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria, Kitambulisho cha Taifa au Leseni ya Udereva
 • Mkataba wa ajira na stakabadhi za malipo ya mshahara
 • Barua ya mwajiri wako kuridhia kupitisha mshahara wako NBC
 • Nakala ya cheti cha ndoa kwa maombi ya mikopo ya pamoja kwa wanandoa
 • Nakala ya hati ya umiliki
 • Uthibitisho wa malipo ya awali ambayo umeshampatia muuzaji wa nyumba
 • Nakala ya Kitambulisho cha mfanyakazi
 • Ripoti ya uhakiki wa nyumba
 • Ripoti ya uthamanishaji wa nyumba
 • Mkataba wa Mauziano (Kama wewe si mteja wa NBC)

Zingatia: Bima ya maisha na bima ya nyumba ni za lazima katika kupata Mkopo wa Kununua Nyumba. Tupo tayari kukusaidia kupata aina yoyote ya bima unayohitaji kupitia kitengo cha Bima cha NBC 

Mkopo wa Nyumba wa NBC inakuwezesha:
 • Kubadili hati umiliki kabla ya kumlipa muuzaji
 • Hati ya umiliki kuandikwa kwa jina lako
 • Kurejesha mkopo kwa kushirikiana na mwenza wako
 • Uhuru wa lipa mkopo kwa kipindi cha hadi miaka 20
Taarifa muhimu
 • Unatakiwa uwe raia wa Tanzania
 • Unatakiwa uwe  mwajiriwa mwenye kulipwa mshahara

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC