Siku zote tunakusudia kutoa huduma bora zaidi. Hata hivyo, wakati mwingine, mambo hayaendi vizuri kama tulivyopanga na tunapenda utujulishe pale ambapo hujafurahia huduma au bidhaa zetu. Kwa kuwasilisha malalamiko yako, unatuwezesha kutatua tatizo lililopo na kuboresha huduma zetu kwako na kwa wateja wetu wote.

Tuna dhamira ya dhati kuyapitia malalamiko yote vizuri na kwa haraka na tunakusudia kuyatatua pale tu yanapotufikia. Tutaendelea kuwahabarisha wateja wetu na kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa taratibu za sheria na kanuni zinazotuongoza.

Baadhi ya viwango vyetu vya kushughulikia malalamiko

Jinsi ya kuwasilisha malalamiko NBC
 • Kuwasilisha malalamiko yako tafadhali nenda kwa mfanyakazi wa NBC kwenye sehemu ya utoaji huduma kwa wateja katika tawi la NBC ulilotembelea au piga simu kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba zifuatazo
  +255 768 984 000; +255 225 511 000 au +255 222 193 000 au kwa baruapepe contact.centre@nbc.co.tz au jaza fomu ya maoni kupitia tovuti hii www.nbc.co.tz
Tafadhali tambua kuwa taratibu zifuatazo zitafuatwa:
 • Mfanyakazi wa NBC atahitaji taarifa muhimu kutoka kwako na kuzihakiki
 • Mfanyakazi wa NBC atakupatia namba ya kumbukumbu ya malalamiko yako na utajulishwa siku ambapo malalamiko
 • yako yatakuwa yameshughulikiwa
 • Mawasiliano kati yako na NBC kuhusiana na utatuzi wa malalamiko yako yatafanywa kupitia baruapepe, njia ya posta au njia ya simu
Hujaridhishwa na suluhisho ulilopewa?
 • Kama hautaridhishwa na suluhisho utakalopewa, tawi husika la NBC litawasilisha kutoridhishwa kwako kwenye kitengo kinachoshughulikia malalamiko ya wateja kilichopo makao makuu ya NBC. Na kama bado hautaridhishwa na suluhisho unaweza kuwasiliana na wakurugenzi wafuatao:

Na kama bado hautaridhishwa na suluhisho kutoka NBC, au haujapokea majibu ya malalamiko yako ndani ya siku 21 za kazi toka ulipowasilisha malalamiko unaweza kupeleka malalamiko yako kwenye Dawati la usuluhishi wa malalamiko ya wateja la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ndani ya siku 14 za kazi. Kama ni suala lenye utata, utaongezewa siku zisizozidi 14 za kazi.

Ili malalamiko yaweze kutatuliwa na Dawati, ni lazima yakidhi vigezo vifuatavyo:
 • Malalamiko hayo yawe yamewasilishwa ndani ya kipindi cha siku kumi na nne(14) baada ya NBC kutoa maamuzi, isipokuwa kwenye maswala yenye utata
 • NBC kufanya maamuzi yake au kushindwa kuyapatia ufumbuzi malalamiko yako, isipokuwa kwa masuala yenye utata ambayo yameongezewa siku 14 za kazi
 • Malalamiko ambayo yametokea katika kipindi kisichozidi miaka miwili (2) iliyopita tangu lilipojitokeza.
 • Lalamiko lisiwe linashughulikiwa mahakamani
 • Lalamiko lisizidi kiwango cha shilling za kitanzania million 15
Upatikanaji wa fomu ya malalamiko za BOT:
 • Fomu za malalamiko za BOT zinapatikana kwenye matawi yetu na mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa NBC atakuelekeza jinsi ya kujaza
 • Fomu iliyojazwa na kusainiwa na mlalamikaji inaweza kuwasilishwa Benki Kuu ya Tanzania kwa njia ya posta au faksi namba +255 22 223 4067
 • Malalamiko yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo:

Benki Kuu ya Tanzania,
Dawati la Usuluhishi wa Malalamiko,
Ofisi ya Katibu wa Benki,
Mtaa wa 2 Mirambo,
S.L.P 11884, Dar es Salaam.

Jinsi ya kuwasiliana nasi:
 • Kwa kufika kwenye tawi lolote la NBC lililo karibu nawe
 • Kupiga simu NBC kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba +255 768 984 000 au +255 222 193 000
 • Kutuandikia baruapepe kwenda contact.centre@nbc.co.tz
Gharama:

Kutuma malalamiko, pongezi au maoni ni bure, hata hivyo, kupiga simu huduma kwa wateja kutalipiwa kwa kiwango cha kawaida cha kupiga simu kulingana na mtandao wa simu unaotumia.

Tuma lalamiko

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free)
contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC