Ikinge biashara yako na majanga ya moto, wizi, uharibifu wa mali au akiba, majeraha kwa wafanyakazi au matatizo yoyote.

Professional using a laptop

Zikinge mali zako zote dhidi ya majanga na uharibifu

NBC inatoa bima kwa ajili ya mali za biashara yako dhidi ya majanga au uharibifu unatoweza kusababishwa na majanga mbalimbali.

card with cash
Majanga ya moto na mengine kama hayo

Hii ni kinga kwa ajili ya majanga au uharibifu unaoweza kusababishwa na moto au majanga kama mafuriko, tetemeko la ardhi na migomo. Bima hii ni kwa ajili ya vitu halisi na uharibifu wa vifaa.

Uhalifu

Ni bima ya majanga ya wizi unaosababishwa na wezi wa kuvunja au kuingia na kuiba ndani ya eneo la biashara tu. Uthibitisho utahitajika kuonyesha tukio hilo.

Glob icon
Bidhaa inayosafirishwa

Ni bima inayokukinga dhidi ya upotevu wa bidhaa wakati inasafirishwa ndani ya nchi kwa njia ya barabara au treni.

Glob icon
Fedha

Hii inakinga dhidi ya upotevu au uharibifu wa fedha kutokana na hatari kama vile wizi na uharibifu wowote.

card with cash
Bima ya Safari za Majini

Ni kinga dhidi ya upotevu au uharibifu wa bidhaa zinaposafirishwa ndani na nje ya nchi kutoka kwenye ghala. Unaweza kupatiwa bima ya kila safari unayofanya.

Hatari zozote za biashara

Ni kinga ya upotevu au uharibifu wa vifaa vya biashara vinavyohamishika na vifaa vingine vinavyotumika nje ya eneo la biashara.

Glob icon
Hatari zozote za wafanyakazi wa mkataba

Ni kinga dhidi ya kazi za mkataba na vifaa vya ujenzi. Inahusisha moto na majanga kama hayo, wizi, na madai ya mtu mwingine anayedai kutokana na uharibifu wa mali na majeraha ya mwili.

Glob icon
Vifaa vya umeme

Ni kinga dhidi ya ajali au uharibifu wa kompyuta, kuharibika kwa mashine au vifaa vya umeme, vikiwamo vifaa vilivyounganishwa kwenye umeme.

Usiruhusu uharibifu au kuzima kwa umeme uathiri kampuni yako

Tutakupatia bima inayokukinga dhidi ya uharibifu au kuzima kwa mtambo au mashine, ambako kunaweza kuathiri biashara yako kwa muda murefu na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha.

card with cash
Hatari zozote za mitambo

Ni kinga ya mitambo na mashine za ujenzi dhidi ya uharibifu wowote wa muda mrefu (mfano, ajali kwenye eneo la kazi) na wizi.

Glob icon
Kuzima kwa mashine

Inasaidia katika matengenezo na kubadili vifaa vyovyote vya mitambo na mashine vilivyoharibika kutokana na tukio lolote lililotokea.

Pata bima ya kukukinga na madeni unayodaiwa na watu wengine

Kutokana na hukumu zinazotolewa kwenye kesi za jinai siku hizi, mtu hawezi kuendesha biashara bila kuwa na bima nzuri ya madeni.

card with cash
Madeni ya mwajiri

Hii itakuinga dhidi ya madeni halali ya biashara pale inapotokea mfanyakazi ameumia wakati akiwa anaendelea na kazi. Hii ni bima ya dharura kwenye mazingira ambayo mwajiri anashitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi, pale ambapo matokeo yamekuwa magumu zaidi kuliko inavyotarajiwa kwenye madeni mengine halali kisheria.

Glob icon
Madeni ya umma

Hii ni kinga ya madeni halali kwenye biashara ambayo unapaswa kumlipa mtu mwingine kutokana na ajali, kifo au majeraha yaliyotokea wakati wa biashara yako. Kifo au majeraha yaliyosababishwa na bidhaa hayahusishwi na yatakatiwa kwa bima nyingine.

Vutia wafanyakazi wenye sifa kwa kuwawekea bima ya wafanyakazi

Wape usalama wanaouhitaji wafanyakazi wako kwa kuwakatia bima ambayo itawasaidia mambo yanapoenda vibaya.

card with cash
Ajali kwa mfanyakazi mwenyewe

Hulipa kiasi fulani cha fedha kulingana na kipato cha mfanyakazi na kiwango cha ulemavu uliotokea, hasa katika mazingira ya kifo au ulemavu wa muda au wa kudumu kwa mfanyakazi. Inamkinga mfanyakazi hata awapo nje ya kituo cha kazi.

Glob icon
Fidia kwa mfanyakazi

Ni kinga kwa ajili ya mfanyakazi kwa mujibu wa sheria chini ya Sheria ya Fidia kwa Mfanyakazi.

Ni bima zinazokinga mambo mbalimbali

Tunatoa bima za kumkinga mtu dhidi ya matukio yoyote yale, ili kumsaidia kuwa na amani wakati wote awapo kwenye biashara zako.

card with cash
Hatari za kwenye biashara

Inakinga biashara yako dhidi ya hasara zinazoweza kusababishwa na moto na hatari kama hizo. Uharibifu ulioupata ni mdogo ukilinganishwa na hasara itakayotokana na uharibifu huo.

Glob icon
Bima dhidi ya visasi

Ni kinga dhidi ya upotevu unaoweza kutokana na kisasi au kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wafanyakazi wako (matatizo haya hayamo kwenye bima ya uhalifu). Ikitokea mfanyakazi amemsaidia mtu mwingine kuiba, hii inachukuliwa kuwa ni kusudio la wizi unaofanywa na mfanyakazi na inashughulikiwa na bima hii.

Tunakurahisishia namna ya kuwasilisha madai

Pakua fomu hapa, ijaze na wasilisha ndani ya siku 7 baada ya tukio, ukiambatisha nyaraka zote muhimu na maelezo, nasi tutashughulikia mara moja.

Vifaa vya kielektroniki
 • Muhtasari wa polisi unaoeleza kuhusu tukio la wizi au moto
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Ripoti ya kitaalamu kwenye mazingira ya uharibifu wa vifaa vya umeme
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile akanara na risiti mbalimbali
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Hatari zozote kwa wafanyakazi

Ajali kwa wafanyakazi
 • Cheti cha matibabu
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya tatizo
 • Muhtasari wa polisi kwa ajali na kifo cha ajali ya barabarani
 • Cheti cha kifo kwa mambo kama haya
 • Stakabadhi ya malipo kwa wanaodai ndani ya mwezi mmoja kabla ya ajali
 • Stakabadhi za gharama za hospitali na matibabu kwa ujumla

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Moto na majanga kama haya
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali

Pakua fomu ya madai (PDF)

Uhalifu
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali
 • Picha ya uthibitisho pale inapolazimu

Pakua fomu ya madai (PDF)

Hatari zozote za biashara (vifaa vya ofisi/biashara)
 • Muhtasari wa polisi unaoeleza kuhusu wizi au moto
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Ripoti ya kitaalamu kwenye mazingira ya uharibifu wa vifaa vya umeme
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile akanara na risiti mbalimbali
 • Nyaraka zinazoonesha kuwapo kwa kitu hicho, kama vile risiti ya manunuzi

Pakua fomu ya madai (PDF)

Usafirishaji wa bidhaa
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti ya manunuzi
 • Kwa ajili ya bidhaa za mtu mwingine: waraka wa madai, waraka wa deni, bili, mkataba wa kumsafirishia biadhaa zake na waraka wa kupakia bidhaa

Pakua fomu ya madai (PDF)

Fedha
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara, risiti na hati ya mauzo

Pakua fomu ya madai (PDF)

Uhandisi
 • Ripoti ya kitaalamu 
 • Kumbukumbu ya matengenezo kutoka kwenye kampuni ya matengenezo
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Bima dhidi ya visasi
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea, namna walivyougundua pamoja na uhakiki na udhibiti uliokuwepo kabla ya upotevu kutokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, nyaraka za mauzo na ukaguzi wa mahesabu
 • Nakala za hati za malipo ya waharifu
 • Hati ya kuachiwa huru kwa waharifu

Pakua fomu ya madai (PDF)

Madeni ya umma
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea
 • Hati ya madai kutoka kwa mtu anayekudai
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Fidia kwa wafanyakazi
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea
 • Muhtasari wa polisi kwa vitu kama ajali au kifo cha ajali ya barabarani
 • Fomu za Ajira zinazotakiwa, kama vile LDI 306 & LDI 307 ‘A’
 • Cheti cha kifo kwa mambo kama hayo
 • Stakabadhi za gharama za hospitali na matibabu kwa ujumla

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Madeni ya mwajiri
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea
 • Maelezo ya polisi kwa ajali na vifo vya barabarani
 • Cheti cha kifo kwa mambo kama hayo
 • Hati ya madai/samasi lazima ziwasilishwe kwetu baada ya kupokelewa na kabla ya kuzijibu

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Kuharibika kwa mashine
 • Hati ya taarifa
 • Muhtasari wa polisi
 • Risiti/Ankara ya manunuzi
 • Maelezo ya thamani yake
 • Ripoti ya uchunguzi
 • Ripoti ya mtaalamu

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Kuathiriwa kwa biashara
 • Hati ya taarifa
 • Muhtasari wa polisi
 • Ripoti ya uchunguzi

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Bima ya safari za majini
 • Hati ya taarifa
 • Muhtasari wa polisi

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Vifaa vya kielektroniki
 • Muhtasari wa polisi unaoeleza kuhusu wizi au moto
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Ripoti ya kitaalamu kwenye mazingira ya uharibifu wa vifaa vya umeme
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti mbalimbali
 • Nyaraka zinazoonesha kuwapo kwa kitu hicho, kama vile risiti ya manunuzi yake

Tafadhali wasiliana na Meneja Mahusiano au tembelea tawi la NBC lililopo karibu yako kwa ajili ya kupata fomu ya madai.

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191

Tuandikie baruapepe:

contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi