Tafadhali pakua hapa fomu ya madai, ijaze na kuituma kwetu ikiwa na nyaraka zote muhimu kama inavyooneshwa hapa chini.

Unapaswa kuleta nini unapowasilisha madai

Hand holding plus sign icon
Gari Langu

Kwa Bima ya Gari

 • Fomu ya madai iliyojazwa
 • Muhtasari wa polisi
 • Nakala ya leseni ya udereva
 • Ripoti ya Uchunguzi/Tathmini ya ajali
 • Nyaraka zinazosaidia kujua kiasi unachodai kama vile ankara ya madai na makadirio ya gharama kutoka gereji
 • Kwenye mazingira ambapo gari limepotea/limeibiwa: Nyaraka za umiliki, kama vile kitabu cha ratiba ya safari/hati ya kulisafirishia/funguo za gari/cheti cha bima
 • Sera ya kulipia gharama za madai, pale inapolazimu kufanya hivyo

Fomu ya Madai

Information - icon
Nyumba Yangu

Bima ya Nyumba

 • Fomu ya madai iliyojazwa
 • Muhtasari wa polisi unaoonesha wizi au moto uliotokea
 • Maelezo ya mashahidi au maelezo ya mwenye bima akielezea tukio hilo
 • Nyaraka zinazosaidia kujua kiasi unachodai au uwepo wa nyaraka kama vile ankara na risiti za malipo

Fomu ya madai ya kuvunjiwa kioo
Fomu ya madai ya moto

Checklist - icon
Maisha Yangu

Viambatisho kwenye madai ya Bima hii

 • Fomu ya madai iliyojazwa
 • Nakala halisi ya hati ya kifo
 • Nakala halisi hati ya mazishi
 • Nakala ya Kadi ya ATM

Fomu ya Madai ya Mwisho
Fomu ya Madai ya Bima ya Maisha

Bima ya Huduma ya Elimu

 • Fomu ya madai iliyojazwa
 • Nakala halisi ya hati ya kifo
 • Nakala halisi hati ya kibali cha mazishi
 • Ripoti ya polisi (kama ni ajali)
 • Taarifa ya matibabu (kwenye ugonjwa)
 • Nakala ya kitambulisho

Tafadhali wasiliana na tawi lililopo karibu yako ili kupata fomu ya madai

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie baruapepe:

NBC_Insurance@nbctz.com

Kata bimaTawi la NBC