Hakikisha unafurahia nyumba yako – hamishia mkopo wako wa nyumba NBC na ufurahie viwango nafuu na masharti nafuu ya urejeshaji.

Ninahitaji Mkopo

Ninapataje Mkopo Kulipia Mkopo wa Nyumba?

Namna ya Kuomba Mkopo wa Kulipia Mkopo wa Nyumba

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana nawe, au tembelea tawi lolote la NBC lililopo karibu nawe.

Vitu vya kuwa navyo unapoomba mkopo huu

 • Nakala ya Kitambulisho kimoja kati ya vifuatavyo:-  Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria, Kitambulisho cha Taifa au Leseni ya Udereva
 • Mkataba wa ajira na stakabadhi za malipo ya mshahara
 • Barua ya mwajiri wako kuridhia kupitisha mshahara wako NBC
 • Nakala ya cheti cha ndoa kwa maombi ya mikopo ya pamoja kwa wanandoa
 • Nakala ya hati ya umiliki
 • Uthibitisho wa malipo ya awali ambayo umeshampatia muuzaji wa nyumba
 • Nakala ya Kitambulisho cha mfanyakazi
 • Ripoti ya uthamanishaji wa nyumba
 • Makataba wa Mauziano (Kama wewe si mteja wa NBC)

Zingatia: Bima ya maisha na bima ya nyumba ni za lazima katika kupata Mkopo huu. Tupo tayari kukusaidia kupata aina yoyote ya bima unayohitaji kupitia Kitengo cha Bima cha NBC

Mkopo wa Kulipia Mkopo wa Nyumba hukupatia:
 • Viwango nafuu vya riba ya mkopo
 • Mikopo ya Fedha ya Kitanzania kati  ya  shilingi milioni 20 hadi 500
 • Hati ya umiliki kuandikwa kwa jina lako kabla ya kumaliza kumlipa muuzaji
 • Kurejesha mkopo kwa kushirikiana na mwenza wako
 • Uhuru wa kurejesha kwa kipindi cha miaka 20
Taarifa muhimu
 • Mkopo wa NBC wa Kulipia Mkopo wa Nyumba hutolewa kwa raia wa Tanzania
 • Unahitaji kuwa mwajiriwa mwenye kulipwa mshahara

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC