Vidakuzi ni nini?

Vidakuzi ni faili za maandishi zilizosalama ambazo seva za wavuti zinaweza kuhifadhi kwenye kompyuta yako wakati unapotembelea tovuti yetu. Vidakuzi vinaiwezesha seva kukutambua wakati mwingine utakapoingia tena kwenye tovuti yetu.

Aina mbili kuu za vidakuzi

clock icon
Vidakuzi vya muda mfupi

Hizi hukaa kwenye kompyuta yako kwa ule muda unaotembelea tovuti yako na zinafutwa wakati wa kuondoka. Zinakutambua unapohama toka kurasa moja ya tovuti kwenda nyingine, kwa mfano kurekodi vitu unavyoongeza kwenye kikapu chako cha manunuzi mtandaoni. Vidakuzi husaidia pia kudumisha usalama matandaoni.

Vidakuzi vya Kudumu

Hizi zinakaa kwenye kompyuta yako mpaka zitakapoish au zimefutwa. Nyingi huundwa moja kwa moja zikiwa na tarehe zitakazofutwa ili kusaidia kuhakikisha kompyuta yako haijai. Vidakuzi hivi mara nyingi huhifadhi taharifa zako za kuingilia mtandaoni, Kwa hiyo huhitaji kukumbuka taarifa zako hizo za uanachama kwenye tovuti husika.

refresh icon
Tunatumia aina zote za Vidakuzi

Zaidi ya hayo, vidakuzi vinaweza kuwa vya tovuti husika au vya wakala wa tovuti hiyo. Vidakuzi vya tovuti husika vinamilikiwa na huundwa na kampuni ya tovuti unayoangalia. Vidakuzi vya wakala vinamilikiwa na zinaundwa na wakala/kampuni wa kujitegemea wa kampuni ya tovuti hivyo,  kwa kawaida kampuni inayotoa huduma kwa wamiliki wa tovuti.

Vidakuzi vina kazi gani

Vidakuzi vya wavuti ni vya kawaida na haviharibu mfumo wa kompyuta yako - vinahifadhi tu au kukusanya taarifa za tovuti. Vinakusaidia kufanya mambo mtandaoni, kama kukumbuka maelezo ya kuingilia kwenye tovuti husika, kwa hivyo huna haja ya kuingia tena na tena kila wakati unaporudi kuitembelea tovuti hiyo.

Tunatumia Vidakuzi kwa

  • Kukusanya maelezo ya safari ya wateja kwenye tovuti yetu ya umma tu
  • Uhifadhi wa muda mfupi wa maelezo ya vikokotoo vya mahesabu, zana na vielelezo
  • Kuhifadhi maelezo ya masoko, mapendekezo ya bidhaa zetu ili kufikia kusudi letu na kuboresha safari yako kupitia tovuti yetu na tovuti za wadau wetu
  • Tathmini ya ufanisi wa matangazo na promosheni zetu

Hatutumii Vidakuzi kwa kufuatilia utumiaji wa wavuti wa watu baada ya kuondoka kwenye tovuti zetu na hatuhifadhi habari binafsi za watu ambazo wengine wanaweza kusoma na kuelewa. Hatuwezi kuuza au kusambaza habari ya vidakuzi bila ridhaa yako kwanza.

Kubadilisha mipangilio ya Vidakuzi vyako

Ili kuruhusu au kuzuia vidakuzi, fuata maagizo yaliyotolewa na kivinjari chako (kwa kawaida iko ndani ya kituo cha 'Msaada', 'Zana' au 'Badili'). Vinginevyo, taarifa nyingine kuhusu vidakuzi na jinzi ya kuvitumia zinapatikana kwenye Yote Kuhusu Vidakuzi

Unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 |+255 (0) 222 193 000 |+255 (0) 225 511 000 | 0800711177 (free)

Tuandikie b-pepe:

contact.centre@nbctz.com
Wasiliana nasi Tafuta tawiai