Masharti na vigezo vinaeleza wajibu wetu kwako na wajibu wako kwetu unapotumia tovuti ya Benki ya Taifa ya Biashara (National Bank of Commerce (NBC) Limited. 
na kujisajili kwenye huduma NBC Online Banking.

 • 1.Fasili

  Katika vigezo na masharti haya fasili zifuatazo zitatumika:

  Wewe” inamaanisha mteja anayetumia tovuti hii.
  Benki, “sisi”, “au” or “yetu” inamaanisha Benki ya Taifa ya Biashara (National Bank of Commerce (NBC) Limited.
  Tovuti” inamaanisha tovuti ya Benki ya Taifa ya Biashara (National Bank of Commerce (NBC) Limited.

 • 2.Masharti ya Tovuti

  Vigezo na masharti haya yamekusudiwa kukuongoza unapotumia tovuti hii. Kwa kuingia katika Tovuti hii, umekubaliana na vigezo na masharti haya. Tafadhali zingatia kwamba kama umefungua akaunti kwetu, vigezo na masharti haya yatatumika pamoja na yale yanayohusiana na akaunti yako.

  Tuna haki ya kubadili vigezo na masharti haya wakati wowote kwa kuyaweka mabadiliko hayo kwenye website hii bila kutoa taarifa.

  Kuendelea kwako kuingia kwenye tovuti hii au kutumia tovuti hii inaashiria kwamba umekubaliana na vigezo na masharti yaliyorekebishwa.

 • 3.Matumizi ya Tovuti hii

  Kwa busara na utashi wa benki tunaweza kukuzuia kuingia au kutumia tovuti hii kwa sababu mbalimbali, bila mipaka, pale tutakapogundua kwamba hujazingatia vigezo na masharti ya tovuti hii.

  Tovuti hii imekusudiwa uingie kwa kutumia ukurasa wa mwanzo. Kuingia ukurasa maalum wa tovuti hii kupitia kiungo (hypertext link) kingine itaashiria kwamba huoni umuhimu wa taarifa za Tovuti hii na masharti yanayohusiana na matumizi yake.

  Wakati tukijitahidi kuhakikisha kwamba inapatikana kwa saa 16 kwa siku (kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki), hatutahusika na lolote ikiwa kwa sababu yoyote ile tovuti hii haitapatikana kwa wakati wote na muda wote.

  Tafadhali kumbuka pia kwamba kuingia kwako kwenye tovuti hii kunaweza kusitishwa kwa muda bila taarifa ili kuruhusu matengenezo au uingizaji wa huduma mpya ufanyike, au kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

  Benki ina haki ya kuboresha Tovuti wakati wowote bila kulazimika kukupatia taarifa.

 • 4.Hakimiliki, haki zote zimehifadhiwa

  Muundo na maudhui yote ya tovuti hii ni mali ya Benki ya Taifa ya Biashara (National Bank of Commerce Limited). Nembo na Jina lake vimesajiliwa kama alama za kibiashara za Benki ya Taifa ya Biashara. Alama zote za kibiashara, majina ya bidhaa, nembo na muundo wa tovuti vilivyomo kwenye tovuti hii ni mali yetu halali kisheria (intellectual property). Haki zetu zote zimehifadhiwa na taarifa zilizomo ni kwa ajili ya usalama wako binafsi.

  Huruhusiwi kupakua (tovuti yote au sehemu yake), kuituma, kunakili, kusambaza au kurekebisha tovuti hii bila idhini ya maandishi kutoka kwetu. Hata hivyo, unaweza kuchapa kwenye karatasi sehemu ya tovuti yetu kwa matumizi yako binafsi.

 • 5.Bidhaa na Huduma za Mtu Mwingine

  Pale tunapotoa kiungo kwenye tovuti za watu wengine, viunganisho hivyo vinatolewa kukupa tu taarifa kwa urahisi.

  Uingizaji wa kiungo chochote isichukuliwe kuwa idhini yetu kwa bidhaa au huduma zilizopo kwenye tovuti hizo. Utumie viungo hivyo kwa hasara zako mwenyewe na hatutawajibika wala kuhusika na maudhui yake, kutumia au kupatikana kwa tovuti hizo au kwa upotevu au uharibifu wowote, unaotokana na matumizi hayo. Hatujathibitisha ukweli na usahihi wa maudhui yoyote ya tovuti hizo.

  Tovuti hii pia inaweza kuwa na taarifa zilizotoka kwa watu wengine na kwa hizo pia hatuhusiki na usahihi wa taarifa hizo. Mtu yeyote haruhusiwi kuunganisha tovuti nyingine na tovuti hii bila kubata idhini ya maandishi kutoka kwetu.

 • 6.Hakuna Kichocheo

  Hakuna kitu chochote kwenye tovuti kinapaswa kuchukuliwa kama kuomba au kutoa rushwa au hongo, au kichocheo au mapendekezo ya kupata au kuondoka uwekezaji wowote au kushiriki katika shughuli nyingine yoyote, au kutoa ushauri au huduma yoyote ya uwekezaji.

 • 7.Hakuna Dhamana

  Japokuwa tunajitahidi kuhakikisha kwamba taarifa zilizotolewa kwenye Tovuti hii ni sahihi na zinaenda na wakati, lakini hatutoi dhamana ya aina yoyote, ya maandishi au ya kuashiria, kuhusiana na usahihi, ubora, uthabiti na ukamilifu wa taarifa hizo. Maoni na maudhui mengine yote kwenye Tovuti hii tumeandaa sisi kwa ajili ya matumizi binafsi na kwa ajili ya taarifa tu na yanaweza kubadilishwa muda wowote bila taarifa. Kama una mashaka yoyote kuhusu usahihi wa taarifa zilizomo kwenye kurasa hizi, tafadhali kuwasiliana nasi kwa kutuandikia barua pepe kwenda contact.centre@nbc.co.tz au kutupigia simu kwa namba +255 768 984 000,+255 (0) 222 193 000 au +255 (0) 225 511 000

 • 8.Hakuna Dhima

  Kadiri inavyowezekana na kwa mujibu wa sheria, hatutahusika  na tukio lolote ikiwamo (bila mipaka) la uzembe, na/au la uharibifu au upotevu wowote, ikiwamo (bila mipaka) wa moja kwa moja, usio wa moja kwa moja, wa ghafla, uharibifu wa matokeo au wa dharura, gharama au upotevu ambao utatokana na wewe au mtu mwingine kutokana na:

  1. Kutumia au kushindwa kwako kutumia Tovuti hii, au kupakua kwako nyaraka zozote kutoka kwenye Tovuti hii au kuhusu tatizo lolote, ufutaji, uharibifu, virusi vya kompyuta (ikiwamo bila mipaka, upotevu au uharibifu unaotokana na virusi ambavyo vinaweza kuingia kwenye kompyuta, programu, data au mali yoyote, au programu kushindwa kufanyakazi), upotevu wa faida, nia njema au sifa njema, hata kama ilielezwa kwa uwazi kuhusu uwezekano wa kutokea kwa upotevu au uharibifu huo, kutokana na au kuhusiana na kuingia, kutumia, kuendesha, kusoma, au kuunganishwa kwenye tovuti nyingine kutoka kwenye Tovuti hii au kitu chochote cha kwenye tovuti.
  2. Tendo lolote linalohusiana na maudhui ya Tovuti hii au matumizi yoyote au matumizi ya maudhui hayo au tatizo au ufutaji unaotokana na uhamishaji wa maudhui ya Tovuti hii.
  3. Kwa matumizi yoyote mabaya ya huduma au Tovuti hii yanayofanywa na mtu mwingine, Benki haitahusika na ubora wa huduma, mwingiliano wowote toka kwenye mtandao wa intanet unaotumia, kampuni ya simu au mtu mwingine yoyote.
 • 9.Kusitishwa kwa Huduma

  Tunayo haki ya kubadili, kuzuia, kuifunga tovuti hii au sehemu ya tovuti hii wakati wowote kwa muda mfupi au moja kwa moja na kukupa au bila kukupa taarifa. Unakubali kuwa hatuna dhamana kwako au kwa mtu mwingine yoyote juu ya mabadiliko hayo, uzuiaji au ufungaji wa tovuti hii.

 • 10.Kusitishwa na madhara ya kusitishwa

  Tuna haki ya kuboresha, kusitisha au kuondoa, kwa muda au moja kwa moja Tovuti hii au sehemu ya Tovuti hii, kwa kutoa taarifa au bila kutoa taarifa, na wakati wowote.

  Unaafiki kwamba hatutahusika kwako au kwa mtu mwingine kuhusiana na mabadiliko, usitishwaji au uondolewaji wa Tovuti hii.

  Majanga ya asili, bila kuathiri masharti yoyote ya Mkataba huu, Benki haitahusika katika kutimiza au katika utekelezaji wowote wa vigezo au masharti ya Mkataba huu ukicheleweshwa au ukizuiliwa kutokana na vurugu au matatizo yoyote ya kiraia; vita; vitendo vya maadui; migomo; uhaba wa vifaa kwa watu wengine, migogoro ya wafanyakazi; uharibifu wa vifaa vya umeme au simu; moto; mafuriko; matendo ya Mungu; matendo ya Serikali au wakala wa viwango; au, bila mipaka, vyanzo vingine vilivyo nje ya uwezo wake, na ambavyo kwa juhudi zetu zote tumeshindwa kuvidhibiti, ama kutokana na aina ya vyanzo vilivyotajwa hapa au la.

  Kama kutatokea majanga yoyote ya asili, tutatoa taarifa ya maandishi kwako na tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu wote kupunguza makali ya athari za tukio hilo.

 • 11.Kutoa Taarifa

  Taarifa na Maelekezo yaliyopokelewa kutoka kwako kupitia kwenye Tovuti hii yatatunzwa na Benki na yatatumiwa na wafanyakazi wa Benki tu kwa matumizi ya benki (kama itaonekana kuwa muhimu).

 • 12.Sheria ya Majanga ya Asili

  Bila kuathiri masharti ya Mkataba huu, Benki haitahusika katika kutimiza au katika utekelezaji wowote wa vigezo au masharti ya Mkataba huu ukicheleweshwa au ukizuiliwa kutokana na vurugu au matatizo yoyote ya kiraia; vita; vitendo vya maadui; migomo; uhaba wa vifaa kwa watu wengine, migogoro ya wafanyakazi; uharibifu wa vifaa vya umeme au simu; moto; mafuriko; matendo ya Mungu; matendo ya Serikali au wakala wa viwango; au, bila ukomo, vyanzo vingine vilivyo nje ya uwezo wake, na ambavyo kwa juhudi zetu zote tumeshindwa kuvidhibiti, ama kutokana na aina ya vyanzo vilivyotajwa hapa au la.

  Kama kutatokea majanga yoyote ya asili, tutatoa taarifa ya maandishi kwako na tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wote kupunguza makali ya athari za tukio hilo.

 • 13.Sheria inayotuongoza

  Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio zitatumika kusimamia vigezo na masharti ya Mkataba huu na unaafiki kwamba Mahakama za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitakuwa na mamlaka yote au kuamua jambo au mgogoro wowote unaohusiana na au unaotokana na tovuti hii na vigezo na masharti haya.

  Tovuti hii imeandaliwa kwa ajili ya kutumika nchini Tanzania Bara na Zanzibar tu na haikusudiwi kusambazwa au kutumiwa na mtu mwingine au shirika katika mamlaka au nchi yoyote pale ambapo uchapishwaji wake au upatikanaje wake au usambazaji huo au matumizi hayo yatakinzana na sheria au kanuni za nchi hiyo.

  Kama utachagua kutumia taarifa zilizomo kwenye tovuti hii, ni wajibu wako kutii sheria za nchi, taifa au za kimataifa pamoja na matumizi yoyote ya Tovuti hii nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa juu yako. Ili kupata mwongozo kuhusiana na mazingira yoyote, tafadhali wasiliana na mshauri wako wa masuala ya kisheria.

  Bidhaa na huduma zilizomo kwenye tovuti hii zimekusudiwa kwa ajili ya wateja waliopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tu.

  Kama kifungu chochote cha vigezo na masharti haya (au sehemu yake) kitaonekana na mahakama au mamlaka yoyote kutofaa, hakitekelezeki au siyo halali kisheria, vifungu vingine vitaendelea kutumika kama vilivyo.

 • 14.Kuwasiliana na sisi kuhusu Tovuti hii

  Maswali au maoni yoyote kuhusu Tovuti hii au kuhusu vigezo na masharti ya Tovuti hii yatumwe kwa barua pepe kwenda contact.centre@nbc.co.tz, kupiga simu kwa namba +255 768 984 000, +255 (0) 222 193 000 au +255 (0) 225 511 000, au njia nyingine zilizoelezwa ndani ya Tovuti hii.

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000
+255 (0) 222 193 000
+255 (0) 225 511 000
0800711177 (free)

Tuandikie:

contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC