Kupitia Mashine za POS za NBC, unaweza kupokea malipo ya bidhaa na huduma zako kutoka kwa mteja wako yeyote mwenye kadi ya VISA. Hii inakupunguzia kazi ya kuhesabu fedha taslimu na hatari ya kuzitunza kwenye eneo lako la biashara hadi utakapopeleka benki.

Inafanyaje kazi

Hand with a tick
Biashara yangu itanufaikaje?
 • Ni njia rahisi na nzuri zaidi kwa wamiliki wa kadi za VISA kulipia bidhaa na huduma mbalimbali
 • Inasaidia kulipia kwa haraka na kwa usalama zaidi
 • Itapunguza upotevu wa fedha kwenye duka lako
 • Itapunguza kuwa na fedha taslimu kwenye biashara
 • Inasaidia kumalizana na malipo kwa haraka – inapunguza foleni na wateja kuwa na furaha
 • Inapunguza safari za benki kwenda kuweka fedha taslimu
 • Inakuthibitishia kukamilika kwa malipo mara moja
 • Unakuwa na uhakika wa malipo kwa miamala yote iliyothibitishwa
 • Inakusaidia kuhakiki kadi ya uongo na iliyofungiwa kwa haraka sana
 • Inakutayarishia ripoti na majumuisho ya mauzo kwenye taarifa ya akaunti yako
atm - icon
Nani anaweza kuwa na Mashine hizi?

Wafanyabiashara ikiwemo:

 • Makampuni yaliyosajiliwa
 • Wabia wabiashara
 • Wamiliki wa Biashara
cash in hand - icon
Vipi kuhusu uhalifu?

Sera ya NBC ya Kuzuia Uhalifu inaelekeza kuwapatia taarifa zote muhimu wafanyabiashara wenye mashine za POS za NBC ili kujiepusha na uhalifu. Halikadhalika, NBC inafuata Kanuni zote za EMV tangu Agosti 2008. 

cash in hand - icon
Ninapeleka maombi wapi?

Wafanyabiashara wenye sifa wanaweza kutuma maombi kupitia kwa Meneja Mahusiano wa NBC, tawi lolote la NBC au kwenye ofisi za NBC.

Mawasiliano:

Idara ya Huduma za Wafanyabiashara
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mtaa wa Sokoine /Azikiwe
Makao Makuu, Ghorofa ya Kwanza
Dar es Salaam

Fax: +255 22 2112367

Ask Expert - icon

Je, unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 222 193 000 | +255 225 511 000 | +255 768 984 000 | 0800711177 (free)

Tuandikie:

NBC_BUSINESSBANKING@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC