• June 2022

    BENKI YA NBC YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 4.5 KWA SERIKALI

    Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Mwigulu Nchemba amepokea gawio la shilingi bilioni 4.5 linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya Benki ya NBC. Serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo.

    Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Nchemba aliipongeza Benki ya NBC  kwa kutoa gawio kwa Serikali na kuakisi mafanikio ya sera ya ubinafsishaji ya serikali iliyolenga kubinafsisha mashirika ya umma ili kuyaongezea tija na ufanisi. “Serikali inajivunia mafanikio ya Benkl ya NBC kwani Benki hii ni moja ya mashirika ya kwanza kabisa kubinafisihwa nchini. Gawio hili la shilingi bilioni 4.5 mnalolitoa leo ni zaidi ya mara tatu ya gawio mlilotoa mara mwisho, hiki ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki yetu ya NBC ipo katika mstari sahihi”, alisema Dkt. Nchemba.

    Waziri Nchemba pia alipongeza Benki ya NBC kwa matokeo mazuri ya fedha ambapo ilipata faida ya shilingi bilionin 60 ambalo ni ongezeko la asilimia 702 kwa matokeo ya mwaka 2020. Vilevile, Waziri Nchemba alipongeza jitihada za Benki ya NBC katika kuchangia maendeleo ya Taifa ikiwamo ulipaji wa kodi ambapo mwaka jana ililipa jumla ya shilingi bilioni 20 kama kodi.

    “Napongeza sana mchango wenu katika uchumi wa taifa. Hakika nyinyi ni mfano wa kuigwa. Uwekezaji wenu katika jamii umekuwa chachu kubwa ya maendeleo. Napongeza sana sera yenu katika msaada kwa jamii ikiwemo uwekezaji katika ligi ya soka ya mpira ya NBC Premier league na uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon ambazo zinalenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya kizazi kwa wanawake” alisema Dkt. Nchemba.

    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi aliishukuru serikali, kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ambazo zimepelekea Benki kufanya vyema sokoni. ”Faida hii ambayo Benki ya NBC imepata na kuwezesha ulipaji huu wa gawaio la serikali, ina akisi mazingira bora ya biashara nchini. Tunajivunia pia kuweza kulipa kodi ya zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka 2021 na kusaidia kupatikana ajira nyingi kupitia uwekezaji wetu katika ligi ya mpira nchini ya NBC Premier league.

    Akizungumzia kuhusu mchango wa Benki kwenye ustawi wa jamii, Sabi alisema” kupitia sera yetu ya msaada kwa jami, tunajivunia kuwekeza katika kutatua changamoto nyingi za jamii ikiwemo uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon zenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya saratani ya shingo za kizazi kwa wanawake” alisema.

    Benki ya NBC ndio mdhamini Mkuu wa ligi ya Mpira Tanzania yaani NBC Premier League.

     

  • May 2022

    Benki Ya NBC Yakutana Na Wateja Wake Mkoani Mbeya, Yatambulisha Huduma Mpya

    Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaelimisha wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.

    Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club, Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki hiyo Bw  Mussa Mwinyidaho alisema benki ya NBC imedhamiria kuboresha huduma zaidi ili wateja wake waendelee kufurahia huduma zilizorahisishwa zaidi ili kuendana na matakwa ya shughuli zao ili waweze kukuza biashara zao.

    “Kupitia NBC Biashara Club tumekuwa na mkakati mpana wa kuwainua wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo wa kibiashara kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka. Mpango huu umekuwa na tija si tu kwa wateja wetu bali pia hata sisi kama benki tumeweza kupata mrejesho uliotuwezesha kuboresha huduma zetu kwa ajili yao,’’ alisema.

    Alisema kupitia klabu hiyo, benki hiyo imeweza kutangaza huduma mpya kwa ajili ya wajasiriamali ikiwemo huduma ya ‘Commercial Property Financing’ inayowawezesha wajasiriamali wenye majengo ya biashara kupata mikopo yenye marejesho nafuu sambamba na huduma ya ‘Commercial Asset Financing’ inayowawezesha wajasiriamali hao kukopa mitambo kwa ajili ya biashara na shughuli za ukandarasi.

    “Pia kupitia tukio hili la leo wateja wetu mkoani Mbeya watapata fursa ya kufahamu huduma zetu za mikopo bila dhamana  ikiwepo huduma ya ‘Distributor financing’ inayowawezesha wajasiriamali kupata mikopo ya kusambaza bidhaa zao  bila dhamana pamoja na huduma ya ‘Purchasing Order Financing’ inayowawezesha wajasiriamali kupata mikopo kwa kutumia Hati ya manunuzi yaani LPO ,’’ alisema.

    Zaidi, Mwinyidahao alibainisha kuwa  kupitia huduma ya NBC Biashara Club benki hiyo imeweza kuwakutanisha wanachama wa klabu hiyo na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya biashara zikiwemo taasisi za serikali kama TRA, BRELA, TBS na nyingine nyingi ili kujadili na kutatua changamoto na kupata mafunzo zaidi kwenye masuala muhimu ikiwemo elimu kuhusu kodi.

    Akizungumza kwa niaba ya wateja hao, Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Masoko (TCCIA)  Mkoa wa Mbeya Bw Erick Sichinga, mbali na kuonesha kuunga mkono mapinduzi ya huduma za kibenki kupitia benki ya NBC alisema wafanyabiashara mkoani humo wameridhishwa kwa kiasi kikubwa na mchango wa huduma ya NBC Biashara Club kwa kuwa kupitia klabu hiyo wameweza kupata mafunzo ya kibiashara sambamba na kuelimishwa kuhusu fursa mpya za masoko na biashara.

     “Suala la benki kubuni huduma mpya ni jambo moja ila kuhakikisha huduma hiyo inaeleweka na inatumiwa vema na walengwa ambao ni sisi wateja nalo jambo zuri zaidi. Tunashukuru sana NBC kwa kuwa si tu wanabuni huduma zinazotugusa bali pia wamekuwa wakihakikisha tunapata uelewa wa kutosha kuhusu huduma hizo kupitia huduma hii ya NBC Biashara Club.’’ Alisema

    Alisema hatua hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa imekuwa ikiwawezesha kufanya uamuzi sahihi kuhusu huduma mahususi zinazoendana na aina ya biashara zao,’’ alisema.

     

    Dodoma Marathon 2022

    JUMLA ya Wanawake 9000 nchini wameweza kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi na wanawake 550 wamegundulika na kupatiwa matibabu ya ugonjwa huo.

    Hilo limewekwa wazi na Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi wakati wa uzinduzi wa NBC Dodoma Marathon zitakazofanyika kwa msimu wa tatu mwaka 2022.

    Sabi amesema, Katika kuunga mkono juhudi za mapambano ya kansa ya kizazi kwa Wanawake ' Benki ya NBC imeandaa Marathon iitwayo 'NBC Dodoma Marathon' yenye lengo la kusaidia Wanawake zaidi ya 20,000 wenye kansa ya kizazi.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa marathon hiyo ambayo itafanyika Dodoma Julai 31, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kwa Tanzania pekee ndani ya mwaka wanawake zaidi ya 1000 wanaopimwa wanakutwa na saratani ya kizazi.

    Amesema, ndani ya miaka miwili wameweza kushirikiana na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road na wamefanikiwa kuwachunguza wanawake 9000 na wanawake 550 wakigundulika kuwa na ugonjwa huo na wameweza kupatiwa matibabu na wamepona.

    "Cancer ya Wanawake ni cancer inayoongoza kuua Wanawake wengi zaidi katika nchi zinazoendelea mfano Tanzania kwa mwaka Wanawake 1400 wanaopimwa wanakutwa na saratani ya kizazi na katika hao 1400 zaidi ya asilimia 30 wanapoteza maisha katika miaka mitatu kwasababu wanakosa tiba zinazostahili"

    Aidha Theobald Sabi amesema katika harakati za kupambana na kansa ya kizazi kupitia marathon hiyo, Wana lengo la kupata milioni 200 kwa mwaka huu na katika miaka miwili iliyopita walikusanya jumla ya milioni 300 ambapo fedha zote hizo watazipeleka katika hospitali ya Ocean Road kwaajili ya matibabu ya Wanawake hao wenye kansa ya kizazi;

    "Cancer hii inatibika hivyo sisi kazi yetu ni kufanya Kampeni ya kukusanya pesa, kufanya awareness na lengo letu ni kupata milioni 200 mwaka huu ambazo zitasaidia kuwapa ocean road na kutibu"

    Sabi amesema Muitikio wa watu kushiriki kwenye marathon ni mkubwa ambapo kwa miaka miwili wameshapata zaidi ya watu 4000, na mwaka huu wanategemea kupata zaidi ya  watu 5000

    Aidha, Sabi Lengo ni kutengeneza ufahamu kwamba cancer hii inatibika Wanawake wawe na tabia ya kupima angalau Kila mwaka wakina mama wawe wanajua Afya zao.

    Kwa upande wa Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Kaisalage amesema wanaishukuru Benki ya NBC wa jambo kubwa wanalolifanya la kuhakikisha wanasaidiana na taasisi yao katika kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

    "Tunapenda kuwashukuru NBC na ukiachilia mbali wanatuunga mkono katika kuwapatia matibabu wanawake na katika miaka miwili tumeshirikiana kwa ukaribu mkubwa sana na wanawake 9000 wameweza kuchunguzwa na wengine 550 wamepatiwa matibabu na wamepona,"

     

    "Ugonjwa huu unaanzia pindi msichana anapoanza kushiriki tendo la kujaamini na Uchunguzi wa saratani ya shingo unafanyika kwa mabinti wa kuanzia miaka 14 na kuendelea na bado tunaendelea kutoa elimu kuwa ugonjwa huu unatibika na unapona kikubwa wasiache kufanyiwa uchunguzi,"ameongeza.

     

    NBC Dodoma Marathon imesajiliwa kimataifa ambapo wana cheti kinachotambulika na wamekuwa wakishirikisha wakimbiaji wa kimataifa kutoka ndani na nje ya nchi.

     

    Benki Ya NBC Yaandaa Futari Kwa Ajili Ya Wateja Wake Zanzibar

    Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar, huku Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  akiipongeza benki hiyo kutokana na ushirikiano inaoutoa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kijamii na kiuchumi.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika Hotel Verde , Zanzibar Spika Zubeir alionyesha kuridhishwa na namna benki hiyo inavyoshirikiana na Baraza hilo pamoja na serikali katika kuleta maendeleo visiwani Zanzibar kupitia mipango yake mbalimbali ikiwemo ile inayogusa moja kwa moja ustawi wa jamii pamoja na serikali.

     “Pamoja na yote hayo zaidi niwapongeze NBC kwa kuonesha umuhimu wa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata kwa namna mbalimbali ikiwemo ikiwemo kwa njia hii ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii…tunashukuru,’’ alisema.

    Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi  alisema benki hiyo imeamua kuandaa futari hiyo ili kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

    Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

    “Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo.” Amesema Sabi

    Zaidi alibainisha kuwa benki hiyo ina huduma maalum inayojikita katika kutoa huduma kwa wateja wake wa imani ya Kiislam, ijulikanayo kama Islamic Banking inayopatikana kwenye matawi yote ya benki hiyo ikiendeshwa katika misingi ya dini hiyo ikiwa na huduma mbalimbali ikiwemo akaunti ya La Riba.

    Bw Sabi aliwaomba wale ambao hawajajiunga na benki hiyo kufungua akaunti zao ili waweze kufurahia huduma bora na za kipekee zinazotolewa katika matawi yote ya NBC nchini.

    Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

  • April 2022

    Benki Ya NBC Yaja Na Huduma Ya Bima Ya Maisha na Afya kwa wanamichezo

    Benki ya NBC ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya NBC imezindua huduma mpya ya Bima kwa wanamichezo mahususi kwa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na familia zao ikilenga kuwahakikishia huduma bora za kiafya wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo hususanipindi wanapota majanga ya kiafya.

    Huduma hiyo inayopewa amana na Kampuni za Bima ya Britam na Sanlam inahusisha Bima ya Afya na maisha   itahusisha wachezaji 640 wanaoshiriki ligi kuu ya NBC, benchi la ufundi pamoja na familia zao.

    Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika mapem hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa soka hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alisema pamoja na faida nyingine, bima hizo zitasaidia kuwapa wachezaji uhuru wa kuonyesha vipaji vyao bila hofu ya kupitia wakati mgumu pindi wanapatwa na kajanga uwanjani ikiwemo kuumia.

    “Huduma hii itawapatia wachezaji uwezo wa kupata matibabu bora ndani na hata nje ya nchi pale itakapobidi. Zaidi pia kupitia huduma hii wachezajiwatapata mafao ya kipato pindi mchezaji atakapopata madhara ya kudumu au kupoteza maisha na faida nyingine ni pamoja na wahusika kupata fao la kiinua mgongo pindi watakapo pata ajali na kushindwa kuendelea na mchezo wa soka,’’ alisema.

    Alisema wakiwa kama mdhamini mkuu wa ligi hiyo, Benki ya NBC imejipanga kuhakikisha kwamba udhamini huo unagusa kila eneo linalohusuuboreshwaji wa mchezo huo ikiwemo kuzingatia suala zima la ustawi wa wachezaji ikiwa ni pamoja na suala la afya zao.

    Hatua hiyo ya Benki ya NBC imeungwa mkono na Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti Mhe. Stanslaus Nyongo ambapo kupitia hafla hiyo pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa huduma hiyo muhimu alisema itasaidia kuboresha ubora wa ligi hiyo kwa kuwa wachezaji watacheza wakiwa huru na amani na hivyo kuonyesha viwango bora.

    Kwa upande Rais ws Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na kuipongeza Benki hiyo na kampuni za Bima za Sanlam na Britam kwa huduma hiyo alisema hatua hiyo ni ya kihistoria na kwamba hatua ya wadau hao inaunga mkono mkakati wa shirikisho hilo pamoja na serikali katika kukuza mchezo huo hapa nchini.

    “Kwa hatua hii ya leo nadiliki kusema kwamba Benki ya NBC si tu ni mdhamini wa ligi kuu ya Tanzania Bara bali pia ni mshirika muhimu katika kukuza mchezo huu. Kwa muda mrefu tumekuwa tukipata changamoto za kiafya kwa wachezaji wetu na suala zima la matibabu limekuwa changamoto kutokana nasababu mbalimbali ikiwemo ukata unaozikabili klabu nyingi

    hapa nchini. Kupitia huduma hii tunakwenda kumalizana na changamoto hii…tunashukuru sana wenzetu wa NBC kufanikisha hili,’’ alisema.

    Kwa upande wao Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bima ya Sanlam, Hamis Suleiman pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bima ya Britam Ramond Komangapamoja na kuelezea umuhimu wa huduma ya bima kwa wachezaji nchini pia waliahidi kutoa huduma bora kwa walengwa hao ili waweze kutimiza wajibuwao vema pindi wanapokuwa uwanjani bila kuhifia atma ya afya zao na familia zao pindi wanapokutwa na changamoto za kiafya wakiwa uwanjani.

    Kwa upande wao wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo akiwemo Frank Lukwaro ambae ni Msemaji wa timu ya Polisi Tanzania na Masau Bwire Msemaji Wa Ruvu Shooting walisema hatua hiyo inakwenda kuamsha ari zaidi kwa wachezaji wa ligi hiyo huku wakibainisha kuwa vilabu vingi vinavyoshiriki ligi Kuu vimekuwa vikitumia fedha nyingi katika matibabu ya majeruhi wa timu hivyo huduma hiyo mkombozi kwao.

    “Huduma hii imesubiriwa kwa muda mrefu na sasa imekuja kama mkombozi kwetu na vijana wetu. Vilabu vyetu vingi havina uwezo wa kuwapatia matibabu mazuri wachezaji wetu hususani pale inapohitajika wao kuwasafirisha nje ya nchi kwa ajili ya matibabu…NBC wamekuwa mkombozi kwenye hili tunashukuru sana,’’ alisema.

  • March 2022

    Benki ya NBC kinara wa kuvunja upendeleo eneo la kazi

    08 Machi 2022

    Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani na kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) imeweka wazi azimio la kufikia usawa wa asilimia 50 kwa 50 kwa watendaji wa benki hiyo.

    Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki na kuhudhuriwa na Mtendaji Mkuu Theobadi Sabi na Menejimenti yake sambamba na wafanyakazi wa Benko hiyo.

    Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa NBC Theobadi Sabi amesema asilimia 48 ya wafanyakazi katika benki hiyo ni wanawake.

    Sabi amesema, lengo la NBC ni kufikia usawa katika nafasi za juu za uongozi ambapo kwa sasa ni asilimia 30-33 ua wanawake wana nafasi za juu za uongozi kwenye benki hiyo.

    “Tunatambua kama taasisi kwamba suala la maendeleo ya wanawake lina faida moja kwa moja kibishara, tafiti zinaonesha kwamba taasisi zinazochukua hatua wanawake wanawwza kufanikiwa na zenyewe zimefanikiwa,”

    “kauli mbiu ya mwaka huu ni Kuvunja upendeleo ambapo benki yetu imelenga kuweka usawa wa asilimia 50 kwa 50 na ukizingatia asilimia 48 ya wafanyakazi ni wanawake,”amesema Sabi

    Sabi amesema, wametumia siku ya leo kuzungumza na wafanyakazi wote wa NBC kuhusu masuala mbalimbali ya usawa na kuzindua programu kwa ajili ya wanawake zitakazowawezesha kusimamia usawa katika nafasi za juu za uongozi.

    Ameongeza kuwa, kwa mwaka 2021 asilimia 53 ya wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika utendaji ndani ya benki ni wanawake na wanaamini kuendelea kuwekeza kwenye maendeleo ya wanawake ni kuwekeza mafanikio ya kibiashara.

    Naye Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Nd Bernard Mshana amesema katika siku hii ya wanawake duniani Benki ya NBC imelenga kumuinua mwanamke kwa kuanzisha akaunti mbalimbali za wanawake za Kikundi na Johari zinazomuwezesha kuweka akiba na hazina makato na kila mwisho wa mwezi unapata faida kuanzia asilimia moja hadi saba.

  • May 2021

    BENKI YA NBC YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA (AMCOS) TABORA

    Tabora, 19 Mei 2021 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia huduma yake ya #NBCShambani inayowalenga wateja wanaojishughulisha na kilimo imeongoza semina ya mafunzo kwa viongozi wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi.

    Hafla hiyo ilifunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tabora, Nd Bosco Ndunguru na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Nd Absalom Cheliga na wakulima wa zao la tumbaku kutoka wilaya za Tabora Mjini, Sikonge na Uyui.

    Pamoja na kuendesha mafunzo hayo Benki ya NBC kupitia Meneja wa Wateja Wadogo, Nd Raymond Urassa walitoa zawadi ya pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Solelansabo, Bi Mary James Merrick ili kumsaidia katika shughuli za kuendesha chama na kuwatembelea wakulima. Pamoja na zawadi ya pikipiki hiyo, Benki ya NBC pia ilitoa baiskeli tatu kwa wakulima kutoka kwa vyama vya msingi mbali mbali kama pongezi kwa juhudi za kupata mazao mengikwa msimu uliopita.

    Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo, Nd Bosco Ndunguru aliipongeza Benki ya NBC kwa kuwawezesha na kuwapa mikopo na huduma za kibenki zenye gharama nafuu wakulima wa zao la tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linalochangia pato la mkoa huo. Aidha alitoa rai kwa benki hiyo kuingia kwenye mazao mengine ili kufungua fursa zaidi kwa wakulima wa mazao mengine. “Ni fursa kubwa sana kwa mkulima mmoja mmoja na ambao wako kwenye vyama mkoani kwetu kwa Benki ya NBC kuwa kwenye sekta ya kilimo na wakulima wanatakiwa kuichamgamki waanze kuzalisha kibiashara.” Aliongeza Nd Bosco.

    Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema kwamba Benki ya NBC kupitia NBC Shambani imejipanga vizuri kuwahudumia wateja wake kupitia matawi yake nchi nzima wakulima wa mazao mbali mbali yakiwemo tumbaku, kahawa, parachichi, pamba na chai.

    Akiongelea huduma za kibenki kwa mkulima mmoja mmoja, Nd Urassa alisema kuwa mkulima anaweza kufungua akaunti bila kuwa na kianzio na kuendesha akaunti bila kuwa na makato ya kila mwezi. “Pamoja na fursa ya akaunti za shilingi na dola, akaunti za vyama vya msingi pia hazina makato lakini pia zina gharama ndogo za uendeshaji kupeleka vyama vya Msingi kuendesha shughuli zake kwa gharama nafuu na kuongeza ufanisi.”

    Kwa upande wake mnufaika wa zawadi ya pikipiki na Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Solelansabo, Bi Mary James Merrick aliishukuru Benki ya NBC kwa zawadi hiyo na kusema kuwa itamsaidia katika kuendesha shuguli zake za chama kwa urahisi na ufanisi zaidi. Aidha alipongeza Benki hiyo kwa kutoa huduma zilizo bora na mikopo yenye riba nafuu inayowawezesha wakulima kutimiza mahitaji yao ya pembejeo kwa wakati.

  • March 2021

    TADB, NBC kutoa bilioni 20 kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo katika minyororo ya thamani ya kilimo

    • Zadhamiria kukuza mitaji na kuleta mageuzi katika sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji

    Dar es Salaam. Jumanne, 13 Aprili, 2021. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia katika makubaliano na benki ya biashara NBC kukopesha shilingi bilioni 20 ili kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo wadogo nchini kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuweza kukuza biashara zao na kufanya mageuzi katika sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji.

    Makubaliano haya, yaliyosainiwa leo katika makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam, yataiwezesha benki hiyo kutoa dhamana kwa wakulima watakaoenda kuomba mikopo NBC kufanya shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi kwa riba nafuu ya asilimia kumi na nne (14%) tu. Dhamana hii inaratibiwa na TADB chini ya mfuko maalum wa dhamana kwa wakulima wadogo nchini ‘SCGS’.  

    “Kwa muda mrefu tumeona wakulima wetu nchini wakipata changamoto ya mitaji. Wengi wakilazimika kukopa kwa riba za kibiashara ambapo wengi wao wamekuwa wakipata changamoto ya kuhimili riba hizo kubwa. Hivyo, kama taasisi ya maendeleo ya kifedha, kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, tumeona umuhimu wa kutoa mikopo hii nafuu kwa kushirikiana na NBC ili kuwawezesha wakulima wengi zaidi kupata mitaji,” alieleza Derick Lugemala, Mkurugenzi wa Fedha kutoka TADB.

    Kwa upande wake, Elvis Ndunguru, Mkurugenzi wa Biashara kutoka NBC, alisema kwamba mikopo hiyo watakayokuwa wanatoa kwa dhamana ya TADB itawawezesha kuwakopesha wakulima wadogo mikopo ya mtaji hadi kiwango cha shilingi 50 milioni kwa mkulima mmoja mmoja, shilingi 500 milioni kwa vikundi na vyama vya wakulima, na hadi shilingi 1 bilioni kwa kampuni ambazo miradi yake inawaunganisha na kuwanufaisha wakulima wadogo wengi.

    Akieleza vigezo vya kupata mikopo hiyo, Ndunguru alisema:

    “Ili kukidhi vigezo vya kupata mikopo hii, mkulima au kampuni husika inahitajika kuwa na biashara hai ya kilimo na mwenye kumbukumbu ya taarifa za kifedha. Mikopo hii inapatikana katika matawi yote ya arobaini na saba (47) ya NBC yaliyopo Tanzania bara na Zanzibar. Tunatoa rai kwa wakulima wote wadogo kuchangamkia fursa hii.”

    Pia, Lugemala alisema, lengo la mikopo hii yenye masharti nafuu ni kuchagiza benki za kibiashara na taasisi za kifedha kutoa mikopo zaidi kwa wakulima na kuwezesha ukuaji wa minyororo yote ya thamani yanayohusiana na kilimo, uvuvi na ufugaji nchini.

    “Mpaka Machi 2021, mfuko huu wa dhamana ulikwisha toa mikopo katika miradi ya kilimo, uvuvi na ufugaji yenye thamani ya shilingi bilioni 75 na kuwafikia wanufaikaji zaidi ya 11,000 moja kwa moja na wasionufaika moja kwa moja 755,000. Baadhi ya miradi tuliyowezesha ni pamoja na kwenye korosho, mpunga, kahawa, miwa, mahindi, mihogo, pamba na ufugaji wa kuku,” alifafanua Lugemala.

    Kutokana na taarifa kutoka TADB, mfuko huu wa dhamana ulianzishwa mwaka 2018. Na katika kipindi cha miaka mitatu sasa, TADB imeshashirikiana na benki na taasisi za kifedha kama NMB, CRDB, Azania, Benki ya Posta (TPB), Stanbic, FINCA Microfinance, UCHUMI Commercial Bank, Tandahimba Community Bank (TACOBA), Mufindi Community Bank (MUCOBA) na sasa NBC.

    “TADB inaamini kwamba kupitia mtandao huu wa ushirikiano wa kimkakati, idadi kubwa ya wakulima wadogo watafikiwa na kuwezeshwa,” alisisitiza Lugemala.

    Mwisho

    Benki Ya NBC Yawafunda Wanawake Kuhusu Ubora Wa Bidhaa Na Mikopo

    Dar es Salaam: Machi 8, 2021: Wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara nchini wameshauriwa kuongeza jitiahada zao zaidi katika kuboresha zaidi mawazo ya biashara sambamba na kuongeza ubora za wa bidhaa zao ili kuongeza ushawishi kwa taasisi za kifedha nchini ziweze kuwakopesha kwa urahisi.

    Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku nne, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo alisema taasisi za kifedha zinashawishika zaidi kutoa mikopo kwa kuzingatia ubora wa wazo la biashara na sio jina au jinsia ya mkopaji.

    Alisema hiyo ndio sababu Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kuwaongezea ujuzi wa wajasiriamali hao ili kuboresha mawazo na bidhaa zao ili kuwajengea uwezo utakaowezesha kufanya biashara zao kwa weledi na kutengeneza faida itayowawezesha kurejesha mikopo yao.

    “Ndio maana kupitia wataalamu ambao tunawatumia kutoa elimu kwa wajasiriamali kupitia maonesho kama haya, tumekuwa tukifundisha na kusisitiza sana juu ya umuhimu wa kujenga zaidi majina ya bidhaa zao kuliko majina yao binafsi kwa kuwa taasisi za kifedha zinatazama zaidi biashara zao na sio jinsia wala majina yao binafsi,’’ alisema Consolatha. 

    Pamoja na kudhamini maonesho hayo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pia iliandaa programu kadhaa za mafunzo kwa wajasiriamali ikiwemo kliniki ya biashara kwa kushirikisha taasisi na mamlaka mbalimbali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

    Zaidi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ilitumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mahususi kwa ajili ya wanawake na wajasiliamali zikiwemo akaunti za NBC Kua Nasi na akaunti mpya ya Johari.

    “NBC Kua Nasi ni akaunti maalum kabisa kwa wote wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kama vile mama na baba lishe, wenye maduka ya reja reja, wasindikaji wa vyakula na mazao, bodaboda, wazabuni wa taasisi mbalimbali wakati akaunti ya Johari ni mahususi kwa ajili ya wanawake na inawezesha kuweka akiba kidogo kidogo kwa kianzio cha shilingi 10,000 tu. Akaunti zote hizi hazina makato ya mwezi,’’ alisema.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala ambae taasisi yake ndio iliratibu maonesho hayo pamoja na kuipongeza benki ya NBC pamoja na wadau wengine kwa kufanikisha maonesho hayo, alisema taasisi hiyo kwasasa inaandaa safari ya mafunzo na maonesho ya biashara katika nchi za Oman na Comoro ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kutangaza biashara zao katika mataifa hayo.

    “Baada ya mafanikio kupitia maonesho haya yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani tunatarajia kuwa na safari za maonesho ya biashara zetu katika nchi za Oman na Comoro ili kufungua milango zaidi ya kutangaza biashara zetu nje nchi,’’ alisema.

  • October 2017

    Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC 

    Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NBC, Prisca Ngonyani na Meneja Uhusiano Junken Njunde wakikabidhi maua na zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Shirika ya Ndege za Kijeshi Tanzania, Hamza Said Johari (Kati) kama sehemu ya kusherehekea Mwezi wa Huduma kwa Wateja na kuwashukuru wateja wakuu na wa thamani.

    Mteja wa NBC mwenye mcheshi sana, Bw. Sosthenes Rutta Bruno akipokea zawadi na maua kutoka kwa Mkuu wa Idara ya NBC ya Wateja Binafsi, Prisca Ngonyani (Kati) na Meneja Uhusiano, Bernard Tibaijuka wakati marafiki hawa wawili walipokuwa wakitembelea wateja wakuu na wa thamani wa NBC katika mwezi wa kusherehekea Huduma kwa Wateja.

    Benki ya NBC ikizindua kampeni ya Akaunti ya Akiba ya Malengo 

    Akaunti ya Akiba ya Malengo ni akaunti ya akiba ambayo imekusudiwa kuwasaidia wateja kufikia malengo yao maalum kwa kipindi mahsusi. Kampeni hii itadumu kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 9 Oktoba 2017 hadi tarehe 8 Januari 2018. Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, wateja wanaoweka fedha benki watanufaika na viwango vizuri vya faida na watakuwa na fursa ya kuchaguliwa kupata zawadi. Kupitia kampeni hii zawadi kwa jumla ya washindi 30 zitatolewa mwishoni. Awamu mbili za mashindano zitaendeshwa kwa miezi ya Oktoba na Novemba, ambapo kutakuwa na washindi 24 watakaopokea zawaida za Shilingi milioni 1 za Kitanzania kila mmoja. Mwezi Disemba, kutakuwa na mashindano makubwa ambayo yatalenga kuchagua washindi wakubwa sita watakaoshinda zawadi ya Suzuki Super Carry mpya sita. Kwa zawadi hizi kubwa, washiriki wote wa Akaunti ya Akiba ya Malengo watakuwa na fursa ya kushinda zawadi hizi.

    Benki ya NBC yazindua Akaunti ya Kikundi

    Kiu ya kupata wateja wapya, hasa ambao hawana akaunti benki na kama sehemu ya kutimiza ajenda ya uhusishaji, Benki ya NBC ilizindua akaunti mpya kwa ajili ya vikundi rasmi na visivyo rasmi vya kijamii na kiuchumi inayoitwa Akaunti ya Vikundi.
    Akaunti hii imeanzishwa ili kusaidia kufikia mahitaji ya kimiamala kwa vikundi rasmi na visivyo rasmi kama vile Benki za Jamii (VICOBA), vikundi vya kijamii vya wanawake, vikundi vya ujirani, vikundi vya shule, SACCOS na vingine kama hivyo. Haya ni makundi yanayoundwa na wanakikundi rasmi na wasio rasmi, wenye malengo yanayofanana ya kusaidiana wakati wa shida.
    Akaunti hii hukisaidia kikundi kupata kitabu cha hundi ili kuwezesha udhibiti wa fedha zao pamoja na miamala yao mingine ya kila siku.

  • August 2017

    NBC celebrates turning 50 years – August 2017

    From left to right: Deputy Governor Bank of Tanzania Dr Kibesse, Deputy Finance Minister Hon Dr Ashatu Kijaji, NBC Board Chairman Nehemiah Mchechu, The Vice President H.E. Samia S Hassan and NBC Acting MD Theobald Sabi in a jovial mood during the gala evening.

    Yvonne Chaka Chaka receiving a standing ovation from invited guests and dignitaries for her outstanding performance

    NBC Partners with China Union Pay International

    NBC launched a partnership with China UnionPay, which will allow UnionPay cardholders to transact at NBC ATMs and Point-of-Sale devices across the country as well as throughout the bank's network in Tanzania.
    UnionPay card holders will be able to transact from the bank's network of over 220 ATMs and 165 Point-of-Sale devices through its 95 merchants across the country.
    China UnionPay International has over five billion cardholders globally and is the preferred payment brand for Chinese nationals. With Tanzania projected to receive Chinese tourists in the region of 40,000 in 2017. Tanzania hosts more than 30,000 Chinese nationals, more than 650 state and privately owned organisations spread across various sectors of the economy and undertaking vast infrastructure, manufacturing, tourism, transport, agriculture and telecommunications projects. It is thus pertinent for NBC to provide financial solutions that meet the growing usage of cards. China has proven to be one Tanzania’s largest foreign investors and has helped to create over 80,000 local jobs, and train a large number of management and technical personnel for Tanzania.

  • July 2017

    NBC launches Business Clubs for SMEs - July 2017

    NBC has launched Business Clubs, which trades as NBC B–Club, in Kahama, Mwanza, and Mbeya following a one-day capacity building workshop for entrepreneurs and businessmen and women. One of the NBC B–Club’s main objectives is to provide non-financial support services through business skills training and capacity building to NBC SME customers, as part of NBC’s commitment in supporting them to grow.

    NBC Acting Managing Director Theobald Sabi (centre) greets Vodacom Tanzania Managing Director Ian Ferrao during a function hosted by VTL in celebrating the successful listing on the DSE. Looking on is NBC Director of Retail Banking Filbert Mponzi

    Kahama entrepreneurs taking selfie photos during the launch ceremony of NBC Business Club in Kahama.

  • June 2017

    NBC holds Iftar for customers in Dar es Salaam – June 2017

    Former President H. E Alhaj Ali Hassan Mwinyi giving a word of thanks during an Iftar hosted by NBC for its customers and invited guests. On the left is Theobald Sabi, NBC Interim Managing Director and on the right is Filbert Mponzi NBC director of Retail Banking, followed by former Prime Minister Dr. Salim Ahmed Salim.

    2nd Malengo vehicle handing over event – June 2017

    NBC Head of Lending, Andrew Lyimo (centre), presenting keys to Mrs Rose Richard Getenyi who received a brand new Toyota Double Cabin Pick Up on behalf of her husband, Mr. Lawrence Cletus Njozi. He won the vehicle during the NBC Malengo Account campaign. Looking on is NBC’ss Liabilities Manager, Dorothea Mabonye. The hand-over ceremony was held at the NBC Head Office recently.

  • May 2017

    50 Years Golden Jubilee Celebrations Dodoma – May 2017

    The minister for Finance and Planning, Hon. Dr. Philip Mpango gives a thumbs up in appreciation for the TZS1.2 billion cheque issued by NBC as dividend payment to the government of Tanzania. The hand-over event was held during NBC’s 50 Years Golden Jubilee gala evening in Dodoma. On the left clapping his hands is Nehemia Mchechu, NBC Board Chairman, in the centre is NBC Managing Director Edward Marks and on the right is Mr. Elias Mwakibinga, Deputy Treasury Registrar.

    NBC appointed lead bank in the country’s largest IPO – May 2017

    NBC Acting Managing Director Theobald Sabi (centre) greets Vodacom Tanzania Managing Director Ian Ferrao during a function hosted by VTL in celebrating the successful listing on the DSE. Looking on is NBC Director of Retail Banking Filbert Mponzi

    NBC Acting Managing Director Theobald Sabi introduces NBC Director of Retail Banking Filbert Mponzi to Reenu Verma Vodacom Tanzania’s Business Manager in the MD’s Office. Looking on the right is NBC Head of Global Clients Wilson Nkuzi.

  • March 2017

    Malengo winner – March 2017

    NBC Head of Retail Banking Filbert Mponzi (centre), handing over insurance cover of a brand new Toyota Hilux Double Cabin Pick Up to one of the winners of the 3-month long Malengo Savings Account Campaign, Mr. Aldo Aidan Nsuha at a function in Dar es Salaam yesterday. Looking on is the winner’s wife Mrs. Zenobia Tarimo.

  • February 2017

    Malengo Savings Account Campaign Draw – February 2017

    NBC Head of Retail Banking Filbert Mponzi (centre), speaking in Dar es Salaam yesterday, before the Malengo Savings Account campaign draw for two brand new Toyota Double Cabin Pick Up vehicles that NBC has given out as main prizes to their customers. The Malengo Savings Account campaign was held over a 3 months period and two eventual winners were announced through a draw. He is flanked from left by Dorothea Mabonye, NBC Retail Liabilities manager and from the right Alina Kimaryo, NBC Marketing Manager.

  • January 2017

    Retail Banking Council Awards Night – January 2017

    Jubilant NBC Corporate branch Manager, Mariam Kombo, displays a certificate after she was announced the Bank’s 2016 Best Branch Manager during the ‘NBC Retail Banking Council Awards’ in Dar es Salaam recently. Looking on is NBC Retail Banking Director, Filbert Mponzi.

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 (0) 768 984 000 | +255 (0) 222 193 000 | +255 (0) 225 511 000 | 0800711177 (Toll-Free)

Tuandikie:

NBC_MarketingDepartment@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC