Ikinge biashara yako dhidi ya hasara zitokanazo na majanga ya moto, wizi, uharibifu wa mali au akiba, majeraha kwa wafanyakazi au matatizo mengine yoyote.

Professional using a laptop

Zikinge mali zako zote dhidi ya majanga na uharibifu

NBC inatoa bima kwa ajili ya mali za biashara yako dhidi ya majanga au uharibifu unatoweza kusababishwa na majanga mbalimbali.

card with cash
Majanga ya moto na mengine kama hayo

Hii ni kwa ajili ya majanga au uharibifu unaoweza kusababishwa na moto au majanga kama mafuriko, tetemeko la ardhi na migomo. Bima hii ni kwa ajili ya vitu halisi na uharibifu wa vifaa.

Ujambazi

Ni bima ya majanga ya wizi unaosababishwa na wezi wa kuvunja au kuingia na kuiba ndani ya eneo la biashara tu. Uthibitisho utahitajika kuonyesha tukio hilo.

Glob icon
Bidhaa zilizoko safarini

Ni bima dhidi ya upotevu wa bidhaa wakati inasafirishwa ndani ya nchi kwa njia ya barabara au treni.

Glob icon
Fedha

Ni bima dhidi ya upotevu au uharibifu wa fedha kutokana na hatari zote ikiwemo wizi na uharibifu.

card with cash
Bima ya Safari za Maji

Ni bima dhidi ya upotevu au uharibifu wa bidhaa zinaposafirishwa ndani na nje ya nchi kutoka au kwenda kwenye ghala. Inaweza kutolewa kwa kila safari unayofanya.

Hatari zote za Biashara

Ni bima inayoshughulika na upotevu au uharibifu wa vifaa vya thamani vya biashara vinavyohamishika na vifaa vingine vinavyotumika nje ya eneo la biashara.

Glob icon
Hatari zote za Wakandarasi

Ni bima kwa ajili ya kazi za mkataba na vifaa vya ujenzi. Inahusisha moto na majanga kama hayo, wizi, na madai ya mtu mwingine anayedai kutokana na uharibifu wa mali na majeraha ya mwili.

Glob icon
Vifaa vya umeme

Bima hii ni kwa ajili ya ajali au uharibifu wa kompyuta, kuharibika kwa mashine au vifaa vya umeme, vikiwamo vifaa vilivyounganishwa kwenye umeme.

Usiruhusu uharibifu au kuzima kwa umeme uathiri biashara yako

Tutakupatia bima dhidi ya uharibifu au kuzima kwa mtambo au mashine, ambako kunaweza kuathiri biashara yako kwa muda murefu na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha.

card with cash
Hatari zote za mitambo

Bima kwa ajili ya mitambo ya ujenzi zinazohamishika dhidi ya uharibifu (mfano, ajali kwenye eneo la kazi) na wizi.

Glob icon
Kuharibika kwa Mashine

Inasaidia katika matengenezo na kubadili vifaa vyovyote vya mitambo na mashine vilivyoharibika kutokana na tukio la uharibifu wa mashine.

Pata bima dhidi ya madeni unayodaiwa na watu wengine

Kutokana na hukumu zinazotolewa kwenye kesi za jinai siku hizi, mtu hawezi kuendesha biashara bila kuwa na bima nzuri ya madeni.

card with cash
Madeni ya mwajiri

Hii ni bima dhidi ya madeni halali ya biashara pale inapotokea mfanyakazi ameumia akiwa kazini. Bima hii inasaidia sana kwenye mazingira ambayo mwajiri anashitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi na matokeo ya kesi yamekuwa magumu zaidi kuliko inavyotarajiwa kwenye madeni mengine halali kisheria.

Glob icon
Madeni ya umma

Ni Bima kwa ajili ya madeni halali kwenye biashara ambayo unapaswa kumlipa mtu mwingine kutokana na ajali, kifo au majeraha yaliyotokea katika kufanya biashara. Kifo au majeraha yaliyosababishwa na bidhaa hayahusishwi na yatakatiwa kwa bima ya aina nyingine.

Vutia wafanyakazi wenye sifa kwa kuwa na bima ya wafanyakazi

Wape usalama wanaouhitaji wafanyakazi wako kwa kuwakatia bima ambayo itawasaidia mambo yanapoenda vibaya.

card with cash
Ajali kwa mfanyakazi

Hulipa kiasi cha fedha kilichopangwa kulingana na kipato cha mfanyakazi na kiwango cha ulemavu uliotokea, hasa katika mazingira ya kifo au ulemavu wa muda au wa kudumu kwa mfanyakazi. Inamkinga mfanyakazi hata baada ya masaa ya kazi.

Glob icon
Fidia kwa wafanyakazi

Ni kwa ajili ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria chini ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Ni bima mbalimbali kwa ajili ya matukio tofauti tofauti

Tunakupa bima dhidi ya kila tukio, ili kukusaidia kuwa na amani wakati wote uwapo kwenye biashara zako.

card with cash
Hatari kwenye biashara

Ni bima kwa ajili ya bisahara yako dhidi ya hasara zinazoweza kusababishwa na moto na hatari kama hizo. Uharibifu unaotokea mara nyingi ni mdogo kuliko hasara inayotokea baadae.

Glob icon
Dhamana ya Uaminifu

Ni bima dhidi ya upotevu unaoweza kutokana na wizi au kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wafanyakazi wako (matatizo haya hayamo kwenye bima ya uhalifu). Ikitokea mfanyakazi amemsaidia mtu wa nje kuiba, hii ni inachukuliwa kuwa mfanyakazi sio muaminifu na inashughulikiwa na bima hii.

Tunakurahisishia namna ya kuwasilisha madai

Pakua fomu kwenye website hii, ijaze na iwasilishe NBC ndani ya siku 7 baada ya tukio, ukiambatisha nyaraka zote muhimu na maelezo yanayohitajika, nasi tutaifanyia kazi mara moja.

Vifaa vya umeme
 • Muhtasari wa polisi unaoeleza kuhusu wizi au moto
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Ripoti ya kitaalamu kwenye mazingira ya uharibifu wa vifaa vya umeme
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile akanara na risiti mbalimbali
 • Nyaraka zinazoonesha kuwapo kwa kitu hicho, kama vile risiti ya manunuzi

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Hatari zote kwa Wakandarasi

Ajali kwa wafanyakazi
 • Cheti cha matibabu
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya tukio
 • Muhtasari wa polisi kwa matuko ya ajali ya barabarani au mauaji
 • Cheti cha kifo kwa matukio ya mauaji
 • Stakabadhi ya malipo kwa wanaodai ndani ya mwezi mmoja kabla ya ajali
 • Stakabadhi za gharama za hospitali na matibabu kwa ujumla

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Moto na majanga kama haya
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile akanara na risiti mbalimbali

Pakua fomu ya madai (PDF)

 • Picha ya uthibitisho kuvunjiwa pale inapolazimu

Pakua fomu ya madai (PDF)

Hatari zote za biashara (vifaa vya ofisi/biashara)
 • Muhtasari wa polisi unaoeleza kuhusu wizi au moto
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Ripoti ya kitaalamu kwenye mazingira ya uharibifu wa vifaa vya umeme
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile akanara na risiti mbalimbali
 • Nyaraka zinazoonesha kuwapo kwa kitu hicho, kama vile risiti ya manunuzi 

Pakua fomu ya madai (PDF)

Bidhaa zilisopo safarini
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti ya manunuzi
 • Kwa ajili ya bidhaa za mtu mwingine: waraka wa madai, waraka wa deni, bili, mkataba wa kumsafirishia biadhaa zake na waraka wa kupakia bidhaa

Pakua fomu ya madai (PDF)

Fedha
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara, risiti na hati ya mauzo

Pakua fomu ya madai (PDF)

Vifaa vya uhandisi
 • Ripoti ya kitaalamu 
 • Kumbukumbu ya matengenezo kutoka kwenye kampuni ya matengenezo
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti
 • Maelezo ya shahidi au maelezo ya mwenye bima yakibainisha mazingira ya upotevu uliotokea

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Dhamana ya Uaminifu
 • Muhtasari wa polisi
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea, namna walivyougundua pamoja na uhakiki na udhibiti uliokuwepo kabla ya upotevu kutokea
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, nyaraka za mauzo na ukaguzi wa mahesabu
 • Nakala za hati za malipo ya wahalifu
 • Hati ya kuachiwa huru kwa wahalifu

Pakua fomu ya madai (PDF)

Madeni ya umma
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uharifu ulivyotokea
 • Hati ya madai kutoka kwa mtu anayekudai
 • Nyaraka zinazoonesha kiasi kinachodaiwa, kama vile ankara na risiti

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Fidia kwa wafanyakazi
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna uhalifu ulivyotokea
 • Muhtasari wa polisi kwa vitu kama ajali au kifo cha ajali ya barabarani
 • Fomu za Ajira zinazotakiwa, kama vile LDI 306 & LDI 307 ‘A’
 • Cheti cha kifo
 • Stakabadhi za gharama za hospitali na matibabu kwa ujumla

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Madeni ya mwajiri
 • Maelezo ya kina kutoka kwa mteja wa bima yakieleza namna upotevu ulivyotokea
 • Maelezo ya polisi kwa ajali na vifo vya barabarani
 • Cheti cha kifo kwa mambo kama hayo
 • Hati ya madai / hati za mahakama lazima ziwasilishwe kwetu baada ya kupokelewa na kabla ya kuzijibu

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Kuharibika kwa mashine
 • Barua ya taarifa ya uharibifu
 • Muhtasari wa polisi
 • Risiti/Ankara ya manunuzi
 • Maelezo ya thamani yake
 • Ripoti ya uchunguzi
 • Ripoti ya mtaalamu

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Kuathiriwa kwa biashara
 • Hati ya taarifa
 • Muhtasari wa polisi
 • Ripoti ya uchunguzi

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Bima ya safari za maji
 • Hati ya taarifa
 • Muhtasari wa polisi

Tafadhali wasiliana na tawi la NBC lililopa karibu yako ili kuwasilisha fomu ya madai.

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191 | 0800711177 (free)

Tuandikie baruapepe:

nbc_businessbanking@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC