Je, kuweka akiba kwa malengo maalum? Ukiwa na Akaunti ya NBC Malengo unaweza kuongeza akiba yako kwa kuweka fedha kidogo kidogo, mara kwa mara, na kukusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi. Pia NBC tunakupatia faida kubwa ambayo inakuongezea akiba yako kila mwezi.

 

 

 

Ninafunguaje Akaunti yangu ya NBC Malengo?

Hand holding plus sign icon
Namna ya Kufungua Akaunti ya NBC Malengo

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lililo karibu nawe.

Unahitajika kuwasilisha nini unapofungua akaunti ya NBC Malengo?

Kwa wateja wenye akaunti NBC

 • Barua rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali ya mtaa
 • Nyaraka halisi za kukutambulisha – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura

Kwa wateja wasio na akaunti NBC

 • Picha mbili za rangi
 • Nyaraka halisi za kukutambulisha – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura
 • Uthibitisho wa anuani ya makazi – mojawapo ya nyaraka zifuatazo:
  • Risiti ya malipo ya bili ya bili ya maji au umeme (iliyolipwa ndani ya miezi sita) inayoonesha anuani ya makazi yako
  • Barua ya rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali za mitaa
  • Barua ya mwanasheria  inayoonesha anuani ya makazi yako
 • Kwa wasio raia wa Tanzania: watahitajika kuleta pasi ya kusafiri, kibali cha makazi au kibali cha kufanya kazi nchini
Information - icon
Akaunti ya Malengo hukuwezesha:
 • Kuweka akiba kwa uhuru kwa muda maalum na kwa malengo maalum
 • Haina makato ya kuendeshaji  wa akaunti
 • Kuweka akiba  kiasi chochote na wakati wowote
 • Kuzalisha faida kubwa itokanayo na riba ambayo inakuongezea akiba yako kila mwezi
Checklist - icon
Taarifa muhimu
 • Unaweza kuomba taarifa ya akaunti yako wakati wowote
 • Inakuwekea mipaka ya kutoa fedha ili uweze kufikia malengo yako

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC