Huduma hii ni maalum kwa ajili ya mahitaji ya kibenki ya vikundi rasmi na visivyo rasmi, kama vile VICOBA, SACCOS, wajasiriamali wadogo wadogo, vikundi vya dini na vikundi vya wafanyakazi. Hivi ni vikundi binafsi vinavyoundwa na watu wenye malengo ya kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kijamii na kifedha.

Fungua Akaunti

Faida za kuwa na Akaunti ya NBC Kikundi

Hand holding plus sign icon
Fungua Akaunti ya NBC Kikundi

Jaza fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea lolote ya NBC lililo karibu nawe

Nyaraka zifuatazo zitahitajika:

 1. Katiba ya Kikundi ikiwa na maelezo yafuatayo: 
  • Madhumuni ya kikundi
  • Chanzo cha mapato au fedha za kikundi
  • Namna kikundi kinavyofanya kazi
  • Vigezo vya wanachama kujiunga na kuondoka kwenye kikundi
  • Idadi ya wanakikundi inayotakiwa katika kufanya maamuzi kwa niaba ya kikundi
 2. Kumbukumbu za kikao ambazo zinaeleza yafuatayo:
  • Ridhaa ya wanakikundi kufungua akaunti ya Kikundi NBC
  • Orodha ya viongozi wote wa kikundi na vyeo vyao
  • Orodha ya watia saini watakaokuwa wanaidhinisha malipo
  • Kumbukumbu zilizosainiwa na mwenyekiti na katibu wa kikundi
 3. Orodha ya wajumbe wote ikiwa na taarifa zifuatazo:
  •  Jina kamili la kila mwanakikundi na majukumu yao kwenye kikundi
  • Kazi / shughuli za kiuchumi za kila mwanakikundi
  • Uraia wa kila mwanakikundi
  • Makazi ya kila mwanakikundi
 4. Nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa na viongozi wa kikundi  (Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina):
 • Moja ya nyaraka zilizoorodheshwa hapa chini:
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha mpiga kura
  • Pasi ya kusafiria
  • Kitambulisho cha taifa
 • Uthibitisho wa eneo la makazi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata (WEO)

     5. Nyaraka za watia saini zilizotajwa hapa chini:

 • Moja ya nyaraka zilizoorodheshwa hapa chini:
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Pasi ya Kusafiria
  • Kitambulisho cha Taifa
 • Uthibitisho wa eneo la makazi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata (WEO) au Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO)
 • Picha ndogo 2 za rangi zilizopigwa karibuni
Information - icon
Akaunti ya NBC Kikundi inakupa:
 • Faida nzuri itokanayo na riba
 • Inakuwezesha kuweka fedha taslimu wakati wowote kwa njia ya simu ya mkononi, kwa Wakala wa NBC, mashine za ATM na matawi yetu
 • Kitabu cha hundi kwa ajili ya miamala ya Kikundi
 • Kupata taarifa ya akaunti ya kikundi kwa njia ya simu wakati wowote na popote kupitia Huduma ya NBC Kikundi Mobile
 • Uendeshaji wa akaunti BURE (Hakuna makato)
 • Watia saini kuidhinisha miamala ya kikundi kupitia Huduma ya NBC Kikundi Mobile wakati wowote na popote
 • Watia saini kuhamisha pesa kwenda kwenye akaunti benki au ya simu ya mwanakikundi kwa njia ya simu ya mkononi wakati wowote na popote
Hand with question mark - icon
Taarifa muhimu
 • Wanakikundi wanaweza kuweka fedha kwenye akaunti yao wakati wowote  kupitia huduma za simu ya mkononi (Airtel Money, M-Pesa, Tigo-Pesa na nyinginezo), au ATM za NBC au Kwa Wakala wa NBC
 • Kikundi cha kuanzia watu NNE wanaweza kufungua Akaunti ya  NBC Kikundi
 • Hakuna mipaka kuhusiana na ukumbwa wa kikundi
 • Watia saini wa kikundi watapokea ujumbe wa simu ya mkono kwa kila muamala unaofanyika kwenye Akaunti ya Kikundi chao

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC