Kupitia Mkopo wa Dhamana ya Nyumba unaweza kukopa fedha hadi 85% ya thamani ya nyumba unayomiliki. Hii inamaanisha kwamba, wewe kama mmiliki wa nyumba, mkopo huu unakupatia fedha taslimu unayohitaji kwa ajili ya maboresho ya nyumba, kulipa madeni au kitu chochote unachohitaji kufanya.

 

Ninahitaji Mkopo

 

Ninapataje Mkopo wa Dhamana ya Nyumba?

Namna ya Kuomba Mkopo huu

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi la NBC lililopo karibu nawe.

Vitu vya kuwa navyo unapoomba mkopo huu

 • Nakala ya Kitambulisho kimoja kati ya vifuatavyo:-  Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria, Kitambulisho cha Taifa au Leseni ya Udereva
 • Mkataba wa ajira na stakabadhi za malipo ya mshahara
 • Barua ya mwajiri wako kuridhia kupitisha mshahara wako  NBC
 • Nakala ya cheti cha ndoa kwa maombi ya mikopo ya pamoja kwa wanandoa
 • Nakala ya hati ya umiliki
 • Uthibitisho wa malipo ya awali ambayo umeshamlipa muuzaji wa nyumba
 • Nakala ya Kitambulisho cha mfanyakazi
 • Ripoti ya uhakiki wa nyumba
 • Ripoti ya uthamanishaji wa nyumba

Zingatia: Bima ya maisha na bima ya nyumba ni za lazima katika kupata Mkopo wa Dhamana ya Nyumba. Tupo tayari kukusaidia kupata aina yoyote ya bima unayohitaji kupitia Kitengo cha Bima cha NBC

Mkopo wa Dhamana wa Nyumba wa NBC unakuwezesha:
 • Kufanya ukarabati wa nyumba yako, kutimiza hitaji lako la fedha au kulipa mkopo wa nyumba unaodaiwa sehemu nyingine
 • Kukopa hadi 85% ya Thamani ya nyumba yako
 • Hati ya umiliki itaendelea kuwa na jina lako
Taarifa muhimu
 • Mkopo wa Dhamana ya Nyumba hutolewa kwa raia wa Tanzania tu
 • Mkopo wa Dhamana ya Nyumba hutolewa kwa wale wanaopata mshahara kila mwezi

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC