Kupitia Mkopo wa NBC Cash Cover, unaweza kupata mkopo wa fedha za Kitanzania hadi 90% ya kiasi cha fedha kilichopo kwenye akaunti yako ya NBC na kuurejesha ndani ya kipindi cha miezi 12.

 

Ninawezaje kupata Mkopo wa NBC Cash Cover?

Namna ya kuomba Mkopo NBC Cash Cover

Jaza tu Fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lililopo karibu yako.

Vitu vya kuwa navyo unapoomba mkopo huu

  • Barua iliyosainiwa na kupigwa muhuri na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wako
  • Andika barua ya maombi, ambatanisha na picha yako ndogo ya rangi
  • Nakala ya Kitambulisho kimoja kati ya vifuatavyo:: - Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria, Kitambulisho cha Uraia au Leseni ya Udereva. Barua ya Utambulisho kutoka kwa mwajiri wako
  • Stakabadhi zinazoonyesha mshahara wako wa miezi mitatu iliyopita
  • Taarifa ya akaunti yako ya miezi sita iliyopita
  • Leseni ya biashara kutoka BRELA (kwa waliojiajiri)
  • Mkataba wa ajira (kwa waajiriwa wa mkataba tu)
  • Taarifa ya akaunti yako kwa miezi 12 (kwa wasio waajiriwa wa mshahara)
Mkopo wa NBC Cash Cover utakuwezesha kupata:
  • Mkopo kulingana na kiasi cha fedha kilichopo kwenye akaunti yako ya NBC
  • Mkopo ambao utaulipa ndani ya muda mfupi sana
  • Fedha taslimu kwa ajili ya mahitaji yako
  • Unafuu na wa  muda na kiasi cha marejesho
Taarifa Muhimu
  • Kwa makubaliano maalum ya riba, unaweza kuchukua fedha zaidi ya uliyoweka kwenye Akaunti yako (Overdraft)

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC