Jipatie fedha kila unapozihitaji. Kupitia Mkopo wa NBC kwa Waajiriwa, utakuwa na amani ya moyoni hasa ukizingatia kwamba mkopo wako unalipiwa bima itakayokusaidia endapo utapata majanga kama kifo, ulemavu wa kudumu na/au kupunguzwa kazi.

 

 

Ninawezaje kupata Mkopo wa Waajiriwa?

Namna ya Kuomba Mkopo wa Wafanyakazi

Jaza tu Fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au unaweza kutembelea tawi lolote la NBC lililopo karibu nawe.

Unapaswa kuleta nini unapoomba mkopo huu?

 • Barua iliyosainiwa na kupigwa muhuri na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wako
 • Andika barua ya maombi, ambatanisha na picha yako ndogo ya rangi
 • Nakala ya Kitambulisho kimoja kati ya vifuatavyo:: - Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria, Kitambulisho cha Uraia au Leseni ya Udereva.
 • Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri wako
 • Stakabadhi zinazoonesha mshahara wako wa miezi mitatu iliyopita
 • Taarifa ya akaunti yako ya benki ya miezi sita iliyopita
 • Mkataba wa Ajira (kwa wafanyakazi wa mkataba tu)
Mkopo wa NBC kwa Waajiriwa unakupa:
 • Fedha taslimu za kugharamia mahitaji binafsi
 • Unafuu wa muda na kiasi cha marejesho
 • Bima itakayokusaidia endapo utapatwa na kifo, ulemavu wa kudumu na/au kupunguzwa kazi
Taarifa muhimu
 • Mkopo huu unapatikana kwa waajiriwa tu wa umma au mashirika / taasisi binafsi
 • Urejeshaji wa mkopo ni kwa makato ya kila mwezi kwa kipindi chote cha mkopo
 • Muda wa kurejesha mkopo ni kati ya miezi 12 hadi 72 

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC