Kufungua akaunti kwa ajili ya mtoto wako au mtu unayemlea ni zawadi ya maisha. Akaunti ya NBC Chanua ipo kwa ajili ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 na inakupa faida itokanayo na riba.

 

Nataka kuweka akiba

 

Faida za kuwa na Akaunti ya NBC Chanua

Hand holding plus sign icon
Namna ya kufungua Akaunti ya Chanua

Jaza tu fomu hii  nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lililopo karibu nawe

Unapaswa uwe na nini unapofungua akaunti

Kwa wateja wa NBC

 • Cheti cha kuzaliwa cha mtoto
 • Barua ya rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali za mitaa
 • Nyaraka halisi za kumtambulisha mzazi au mlezi – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha Taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura

Kwa wateja wasio na akaunti NBC

 • Cheti cha kuzaliwa cha mtoto
 • Picha mbili za rangi zilizopigwa karibuni za mtoto na mzazi au mlezi
 • Nyaraka halisi za kumtambulisha mzazi au mlezi – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha Taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura
 • Uthibitisho wa anuani ya makazi – mojawapo ya nyaraka zifuatazo:
  • Risiti ya malipo ya kodi ya makazi (iliyolipwa ndani ya miezi sita) inayoonesha anuani ya makazi yako
  • Barua ya rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali za mitaa
  • Barua ya mwanasheria ikiainisha wazi makazi yako
 • Kwa wasio raia wa Tanzania: watahitajika kuleta pasi ya kusafiri, kibali cha makazi au kibali cha kufanya kazi nchini
Information - icon
Akaunti ya Chanua inawezesha:
 • Kupata Faida itokanayo na riba
 • Kuweka Akiba BURE bila makato ya kila mwezi ya kuendesha akaunti
 • Kuweka fedha kwenye akaunti yako wakati wowote kupitia huduma za kidigitali
 • Kuhamisha fedha kutoka kwenye simu yako ya mkononi kwenda kwenye akaunti ya benki ya mtoto wako
Checklist - icon
Taarifa muhimu
 • Akaunti ya NBC Chanua ni ya watoto mwenye umri chini ya miaka 18 tu
 • Unaweza kutumia huduma za NBC kwa Njia ya Simu ya Mkononi au Huduma za Kibenki kwa Njia ya Mtandao, Mashine za ATM, mawakala wa NBC unapotaka kuweka fedha kwenye akaunti ya mtoto wakati wowote na popote pale utakapokuwa

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC