Njia rahisi ya kupata taarifa za akaunti yako na na kujua miamala yote inayofanyika kwenye akaunti zako za NBC.

statement icon
Taarifa za kielektroniki

Achana na mfumo wa kupokea taarifa za akaunti yako kwenye makaratasi na uanze sasa kupata taarifa za akaunti yako kwa njia ya baruapepe.

mobile icon
Taarifa kwa njia ya ujumbe wa Simu ya Mkononi

Fahamu kinachofanyika kwenye akaunti yako ya NBC kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kila muamala unapofanyika.

confirm - icon
Faida za taarifa za kielekroniki
  • Taarifa za kielektroniki ni bure
  • Utapokea taarifa yako haraka kuliko ikitumwa kwa njia ya posta
  • Ni salama. Taarifa yako itawasilishwa kwa waraka ulio katika muundo wa PDF na utahitaji Namba ya Siri kuufungua
  • Utapokea taarifa ya akaunti yako mahali popote utakapokuwa duniani
mobile - icon
Nifanyeje ili niweze kujisajili kwenye huduma hii?
  • Jaza fomu ya usajili kisha uilete kwenye tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe
  • Utahitajika kuja na Kitambulisho chako kimoja kati ya hivi: – Kitambulisho cha mpiga kura, Kitambulisho cha Taifa, Passi ya kusafiria au Leseni ya udereva
  • Tafadhali hakikisha kwamba anuani yako ya baruapepe iko sahihi na inafanya kazi
mobile - icon
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Taarifa ya kielektroniki ni nini?

Hii ni nakala ya taarifa ya miamala ya akaunti yako ya NBC inayotumwa kwako kwa njia ya baruapepe.

Nani anastahili kupata taarifa ya kielektroniki?

Wateja wote wa NBC wanastahili kupata.

Mteja anapaswa kufanya nini ili kujisajili kwenye huduma hii?

Jaza fomu ya usajili kisha uilete kwenye tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe

Tafadhali hakikisha kwamba anuani yako ya baruapepe ni sahihi na inafanya kazi.

Je, kuna gharama yoyote kwa huduma hii?

Hapana, huduma hii inatolewa BURE.

Je, umesahau Namba yako ya Siri?

Tafadhali angalia baruapepe uliyotumiwa sambamba na taarifa yako ya kielektroniki. Kwa msaada zaidi au piga +255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000

Je, wateja wataendelea kupokea taarifa kwa njia ya posta?

Mara tu mteja anapojiandikisha kupokea taarifa ya kielektroniki, atakuwa anapokea taarifa hizo kwa njia ya baruapepe.

Je, ninaweza kupokea taarifa yangu ya kielektroniki kwenye anuani zaidi ya moja za baruapepe?

Ndiyo. Unachotakiwa kufanya ni kujiandikisha kwa kuorodhesha anuani zako zote za baruapepe unazotaka zipokee taarifa zako.

Kumbuka: Wateja ambao wamejiandikisha kupokea taarifa za kielektroniki, iwapo watahitaji taarifa kwa njia ya karatasi, wanaweza kuwasilishwa maombi kwenye tawi lolote la NBC au kituo chetu cha huduma kwa wateja na watatakiwa kulipia taarifa hizo.

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free)

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC