Ifanye fedha yako ikuzalishie faida. Ukiwa na Akaunti ya Akiba ya NBC, kiwango chako cha faida kitaongezeka kadiri salio lako linavyoongezeka. Kwa hiyo, kadiri salio lako linavyokuwa kubwa, ndivyo faida pia inavyoongezeka

Ninataka kuweka akiba

Faida ya kuwa na Akaunti ya Akiba ya Kawaida NBC

Hand holding plus sign icon

Namna ya Kufungua Akaunti ya Akiba ya Kawaida ya NBC

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe au tembelea tawi lolote la NBC lililo karibu nawe

Unapaswa uwe na nini unapotaka kufungua akaunti hii

Kwa ambao tayari ni wateja NBC

 • Barua rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali ya mtaa
 • Nyaraka halisi za kukutambulisha – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura

Kwa ambao sio wateja wa NBC

 • Picha mbili za rangi zilizopigwa karibuni
 • Nyaraka halisi za kukutambulisha – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura
 • Uthibitisho wa anuani ya makazi – mojawapo ya nyaraka zifuatazo:
  • Risiti ya malipo ya bili ya maji au umeme (iliyolipwa ndani ya miezi sita) inayoonesha anuani ya makazi yako
  • Barua rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali za mitaa
  • Barua ya mwanasheria inayoonesha anuani ya makazi yako
 • Kwa wasio raia wa Tanzania: watahitajika kuleta pasi ya kusafiri, kibali cha makazi au kibali cha kufanya kazi nchini
Information - icon
Akaunti ya Akiba ya Kawaida Inakupa:
 • Faida itokanayo na riba
 • Njia nzuri na rahisi za kuweka akiba ya fedha zako
 • Kutumia huduma za ATM za NBC muda wowote au mawakala wa NBC nchini
 • Kutumia Huduma za kibenki kwa njia ya intaneti kwa saa 24 popote duniani
 • Kuweka oda ya kuhamisha fedha kielekroniki
 • Kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao
 • Kuhamisha fedha kutoka kwenye simu ya mkononi kwenda kwenye akaunti ya benki
Checklist - icon
Taarifa muhimu
 • Hakuna mipaka ya idadi ama kiasi cha kutoa fedha kutoka kwenye akaunti yako

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC