Siku zote tunakusudia kutoa huduma bora zaidi. Hata hivyo, wakati mwingine, mambo hayaendi vizuri kama tulivyopanga na tunapenda utujulishe pale ambapo hujafurahia huduma au bidhaa zetu. Kwa kuwasilisha malalamiko yako, unatuwezesha kutatua tatizo lililopo na kuboresha huduma zetu kwako na kwa wateja wetu wote.

Tuna dhamira ya dhati kuyapitia malalamiko yote vizuri na kwa haraka na tunakusudia kuyatatua pale tu yanapotufikia. Tutaendelea kuwahabarisha wateja wetu na kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa taratibu za sheria na kanuni zinazotuongoza.

Baadhi ya viwango vyetu vya kushughulikia malalamiko

Jinsi ya kuwasilisha malalamiko NBC
Tafadhali tambua kuwa taratibu zifuatazo zitafuatwa:
  • Mfanyakazi wa NBC atahitaji taarifa muhimu kutoka kwako na kuzihakiki
  • Mfanyakazi wa NBC atakupatia namba ya kumbukumbu ya malalamiko yako na utajulishwa siku ambapo malalamiko
  • yako yatakuwa yameshughulikiwa
  • Mawasiliano kati yako na NBC kuhusiana na utatuzi wa malalamiko yako yatafanywa kupitia barua pepe, njia ya posta au njia ya simu
Hujaridhishwa na suluhisho ulilopewa?
  • Kama hautaridhishwa na suluhisho utakalopewa, tawi husika la NBC litawasilisha kutoridhishwa kwako kwenye kitengo kinachoshughulikia malalamiko ya wateja kilichopo makao makuu ya NBC. Na kama bado hautaridhishwa na suluhisho unaweza kuwasiliana na wakurugenzi wafuatao:
  • Mkuu wa Masoko: David.Raymond@nbc.co.tz
  • Mkurugenzi wa Uendeshaji: Alelio.Lowassa@nbc.co.tz
  • Mkurugenzi Mtendaji: NBCManagingDirector@nbc.co.tz
  • Mkurugenzi wa Wafanyakazi: msafiri.shayo@nbc.co.tz
  • Na kama bado haukuridhishwa na suluhisho kutoka NBC,au haujapokea majibu ya malalamiko yako ndani ya muda ulioanishwa katika kanuni zinamzolinda mtumiaji wa huduma za kifedha, unaweza kupeleka malalamiko yako kwenye Dawati la usuluhishi wa malalamiko ya wateja la Benki kuu ya Tanzania (BOT) ndani ya siku 14 za kazi.
Jinsi ya kuwasilisha lalamiko BOT:
Jinsi ya kuwasiliana nasi:

Tumia njia zifuatazo kuwasilisha lalamiko lako BOT

Tafadhali fika kwenye tawi lolote la NBC
Piga simu NBC kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba +255 768 984 000 au +255 222 193 000 au 0800711177 (Bila Malipo)

Gharama
Kutuma malalamiko/pongezi au maoni ni bure hata hivyo, kupiga simu huduma kwa wateja kutalipiwa kwa kiwango cha kawaida cha kupiga simu kulingana na mtandao wa simu unaotumia
Tuma Malalamiko

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free)
contact.centre@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC