Msaidizi wetu Pendo amezeshwa na teknolojia kukusaidia mteja kupata majibu ya maswali yako kuhusu huduma zetu mahali popote na wakati wowote. Unaweza kuanza kumuuliza maswali Pendo kwa kubofya kitufe kilichopo upande wa kulia chini ya ukurasa huu.
Naanzaje kuwasiliana na Pendo?

Mimi sio binadamu, lakini ninaweza kukusaidia
Pendo anaweza kukujibu maswali rahisi kuhusu huduma za benki masaa 24, siku saba za wiki. Zifuatazo ni namna ambazo Pendo anaweza kukusadia leo.

Huduma na taratibu
Pendo anaweza kukujulisha ni huduma gani zinazokuhitaji kufika tawi la NBC na zile ambazo unaweza kuzipata kupitia simu, mtandao au Aplikesheni ya NBC.
Pendo anaweza kukujibu maswali yanayojitokeza mara kwa mara kama vile ufanye nini ikiwa umepoteza kadi yako ya benki au unahitaji kuboresha taarifa zako za makazi.

Taarifa za huduma na jinsi ya kuzitumia
Pendo anaweza kukujibu maswali yanayojitokeza mara kwa mara kama vile, ni jinsi gani unaweza kupata huduma za kibenki. Kupitia simu yako.
Endelea kufuatilia ukurasa huu!
Pendo ana tabia ya kuendelea kujifunza na kuboresha namna ya kujibu maswali kadiri unavyozidi kumtumia ili kuboresha huduma zake kwako mteja wetu.
Pendo ni nini?
Pendo ni jukwaa la mawasiliano linalowezesha kiteknolojia kupokea na kujibu maswali ya wateja kwa haraka na kwa majibu ya uhakika na maalum kwa mteja husika.
Lengo letu ni kutoa suluhisho la haraka na njia ya mteja kujihudumia mwenyewe ambapo kwa kufanya hivi tutaboresha namna ya kuhudumia wateja wetu.
Pendo anaendelea kujifunza na hivi punde ataweza kutoa msaada kwa mambo yahusuyo akaunti yako ya benki.
Je, Pendo anafanyaje kazi?
Pendo anawezeshwa na teknolojia maalum lakini pia mfumo wa usomaji wa kompyuta.
Hii inamaanisha kadiri unavyomuuliza maswali Pendo ndio jinsi unavyojenga mahusiano ambapo kwa mustakabali huu ataweza kuelewa mahitaji yako na kukusaidia kwa urahisi zaidi wakati ujao.
Nawasilianaje na Pendo?
Bofya alama ya Chatboat kwenye ukurasa wa tovuti yetu, kubaliana na vigezo na masharti na uanze kuwasiliana na Pendo kwa lugha ya kiingereza. Jisikie huru kumuuliza Pendo swali lolote la kibenki kupitia njia ya ujumbe mfupi!
Je Pendo ataniuliza maswali kuhusu taarifa zangu binafsi?
Kwa sababu usalama na faragha ya taarifa zako ni muhimu sana kwetu, tumehakikisha Pendo kuwa salama zaidi. Katu, Pendo hatothubutu kukuuliza kuhusu taarifa zako binafsi kama vile, namba ya akaunti, nywila au namba za siri.
Nawezaje kuchati na Pendo kupitia WhatsApp?
Ni rahisi sana!
Unachotakiwa kufanya ni kupakua Aplikesheni ya WhatsApp na kuhifadhi namba +255 745 000 001 kwa jina la Pendo halafu anzisha maongezi kwa kumuandikia “Hello” naye atakujibu.
Nawezaje kuwasiliana na wakala wa huduma kwa wateja wa NBC?
Tafadhali wasiliana na kituo chetu cha huduma kwa wateja kupitia +255 76 898 4000/4011 and +255 22 219 3000 or +255 22 551 1000 ili kuongea na wahudumu wetu rafiki.
Je, unahitaji maelezo au msaada zaidi?
Tupigie:
+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000
Tuandikie: