Boresha biashara zako za usafirisaji bidhaa ndani na nje ya nchi kwa kupitia huduma zetu na mahusiano mazuri ya NBC na benki nyingine zinazoamika duniani. 

 

Faida za mikopo ya biashara za usafirishaji bidhaa ndani na nje ya nchi

card with cash
Mzunguko wa hela

Inasaidia usimamizi mzuri wa mzunguko wa fedha zako.

Glob icon
Gharama

Ni njia nzuri ya mikopo kulinganisha na huduma ya kutoa fedha zaidi ya kiasi ulichonacho kwenye akaunti yako.

Ushindani

Inakuongezea nafasi ya majadiliano na makubaliano.

card with cash
Majadiliano na makubaliano

Unajadiliana na kupata mkataba wa masharti nafuu kuliko washindani wako.

Glob icon
Uwezeshaji

Kuza mtaji wako kwa kupokea fedha za malipo ya awali.

Professional using a laptop

Tutakusaidia kumudu hatari za kifedha zinazoambatana na usafirishaji bidhaa ndani na nje ya nchi

Kupitia mkopo wa Hati ya Mkopo (Letter of Credit), hatari za malipo zinahamishiwa NBC. Unaweza ukafanya majadiliano ya kupunguziwa bei na wanaokuuzia bidhaa au kuomba kusogezewa muda wa kulipa ili kukusaidia kuborasha mzunguko wako wa fedha.

Hati ya Mkopo ya Kuingiza Bidhaa Hati ya Mkopo ya Kuuza Nje Bidhaa

Haya ni makubaliano thabiti yanayofanywa na NBC kama ‘Benki yenye Dhamana ya Kulipa’ unapoiomba imlipe mnufaika au msambazaji wako baada ya kuwasilisha nyaraka zinazohitajika.


Manufaa

 • Usimamizi mzuri wa miamala
 • Hati ya Kudaiwa haitenguliwi, hivyo hakuna masharti wala vigezo (kama vile tarehe ya mwisho ya kutuma mzigo, masharti ya malipo na mahitaji mengine ya nyaraka) vinavyoweza kubadilika isipokuwa kwa makubaliano na Benki Iliyotoa Hati, Benki Iliyothibitisha (kama ipo) na mhusika mkuu kabla haijabadilishwa

Katika mazingira haya, mwombaji au mnunuzi (mteja wako) anakupatia Hati ya Mkopo kutoka kwenye benki yake kuja kwako kupitia NBC (kama benki inayokushauri) na tutangaalia kama ipo sahihi. Kama itakuwa sahihi, tutakushauri hatua za kuchukua.

Manufaa

 • Unakuwa na uhakika wa malipo yako kutoka kwa mnunuzi au wateja utakapowasilisha nyaraka zinazohitajika za madai yako

Tuachie tukusaidie kuboresha mzunguko wa fedha zako

Kupitia Dhamana za NBC una uhakika wa kulipwa hata kama muuzaji au mnunuzi wako atashindwa kutimiza masharti ya mkataba. Benki ya NBC ina aina mbalimbali za dhamana ambazo zinatumika kulipa inapotokea mtu mwingine anashindwa kukulipa. 

benefits - icon
NBC inatoa aina mbalimbali za Dhamana, ikiwamo:
 • Dhamana ya Zabuni
 • Dhamana ya Utendaji
 • Dhamana ya Malipo ya Awali
 • Dhamana za Kusafirisha nje ya nchi
 • Dhamana za Bandari
 • Dhamana ya malipo
 • Dhamana ya uhifadhi wa mizigo

Pokea na fanya malipo kuja nchini na kwenda nje ya nchi kwa usalama zaidi

Jihakikishie usalama wa malipo yako na udhibiti mzuri wa bidhaa zinazotumwa kutoka nje ya nchi kupitia huduma ya malipo ya kusafirishia kuja na kwenda nje.

Mikopo ya Ukusanyaji - Kuingiza Bidhaa nchini Mikopo ya Ukusanyaji kwa ajili ya Kusafirisha bidhaa Nje ya nchi

Mikopo ya Ukusanyaji kwa ajili ya kuingiza bidhaa nchini ni njia salama na ya uhakika ya kununua bidhaa kutoka popote duniani.

Kwa kuwa nyaraka zinasimamiwa na benki, unaweza:

 • Kufanya majadiliano ya kupata masharti nafuu (Mfano, kulipia baada ya siku 30)
 • Unalipia tu wakati bidhaa zako zimeshasafirishwa

Pokea malipo ya bidhaa unazosafirisha kwenda nje ya nchi. Tunahakikisha kwamba wanunuzi wanapokea bidhaa zao tu baada ya nyaraka zao kuwa zimewasilishwa na benki zao.

Ukusanyaji wa nyaraka ni njia salama zaidi katika kufanya malipo kuliko kuwa na akaunti ya biashara kwa sababu:

 • Miamala yote hufanyika kwenye chaneli za benki
 • Nyaraka hutolewa tu baada ya kupokea maelekezo

 

Professional using a laptop

Timiza majukumu yako ya malipo kwa haraka

Kwa kuwa na mkopo wa biashara ya usafirishaji wa NBC, unaweza kudhibiti hatari, kufanya majadiliano ya kupunguza masharti ya mkopo na shinikizo la mzunguko wa fedha zako.

benefits - icon
Mkopo wa Baada ya Kuingiza Bidhaa nchini

Huu ni mkopo wa muda wa mfupi unaokusaidia kutimiza majukumu yako ya kulipia bidhaa.

Manufaa

 • Unakuwezesha kuboresha mzunguko wa fedha
 • Rasilimali fedha inapatikana kwa wingi ili kukusaidia kulipia gharama za bandari, kuhifadhi na kuuza bidhaa
 • Kuwalipa wasambazaji wako wanapowasilisha bidhaa kwako au muda wa malipo unapofika
benefits - icon
Mkopo wa Ankara ya Kuingizia Bidhaa

Pata fedha kwa muda mfupi kwa kutumia ankara za biashara na nyaraka za kusafirishia bidhaa kupitia kwenye miamala benki.

Manufaa

 • Mzunguko mzuri wa fedha
 • Inapunguza gharama ukilinganisha na mkopo wa Overdraft
 • Kumlipa msambazaji anapokuletea tu bidhaa au muda wa mkataba unapofika
benefits - icon
Mkopo wa Hati Kabla ya Ankara

Haya ni malipo ya awali kwa muuzaji yanayofanyika kabla bidhaa hazijasafirishwa.

Manufaa

 • Mzunguko mzuri wa fedha
 • Inapunguza muda wa kufanya miamala
benefits - icon

 

Mkopo wa Kabla ya Bidhaa Kutumwa

Hii ni fedha inayotumwa kwa muuzaji kwa kuzingatia mkataba wa mauzo, hati ya manunuzi au Hati ya Mkopo.

Manufaa

 • Kupata fedha kabla ya kutuma bidhaa
 • Ina gharama nafuu
 • Nafasi ya kujadiliana ili kupata masharti nafuu ya mkataba
 • Inapatikana kwa fedha za kitanzania na za kigeni

 

benefits - icon
Mkopo wa Ankara ya Punguzo la Bei

Mkopo huu unafaa zaidi pale unapokuwa unauza bidhaa zako kwa kutumia akaunti ya wazi na unawapa wanunuzi wako masharti ya mkopo.

Manufaa

 • Unapata fedha ndani ya muda mfupi kwa kutumia ankara za biashara na nyaraka za kusafirishia
 • Inapatikana kwa biashara za ndani nchi na za nje ya nchi

 

benefits - icon
Punguzo kwenye Hatifungani za Kuuza Nje

Inakuwezesha kupata fedha mapema.

Manufaa

 • Inaboresha mzunguko wa fedha
 • Inapunguza mchakato wa biashara

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191 | 0800711177 (free)

Tuandikie baruapepe:

nbc_businessbanking@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC