Jielekeze katika kupanua wigo wa biashara yako na utuachie sisi tukusaidie kuzunguka kwenye vituo vyako vya biashara. Huduma zetu za Kukusanya Fedha zinakusaidia kupokea na kupeleka fedha benki au kwa mtoa mteja wako ambaye anakuuzia bidhaa kwa haraka na usama na kwa gharama nafuu.

 

Professional using a laptop

Uzoefu wetu wa kupeleka fedha kwenye matawi ni thabiti huwezi kuulinganisha popote

Peleka fedha zako kwenye tawi lolote. Tuna matawi nchi nzima.

Ninajiungaje na Huduma za Ukusanyaji Fedha kwenye Matawi ya NBC

Jaza fomu ya maombi au fomu ya maombi kwa njia ya mtandao nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea Tawi la NBC lililopo karibu yako.

Manufaa
 • Ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wasambazaji na watu mbalimbali
 • Ina kuongezea muda zaidi wa kufanya Biashara/kazi
 • Baadhi ya matawi hufunguliwa hata Jumapili
 • Unakuwa na uwezo wa kujua makusanyo yako kwa kutumia huduma za kibenki kwa njia ya mtandao
Taarifa muhimu
 • Inapatikana kwa ajili ya wateja wetu wenye akaunti za kukunyia fedha
 • Pata faida kwenye akaunti yako ya kukusanyia fedha kutegemea na salio lililopo
 • Faida kwenye akaunti yako ya kukusanyia fedha inapatikana kulingana na salio la kila siku
 • Faida italipwa mwishoni mwa kila mwezi
 • Chukua fedha kwenye akaunti yako ya kukusanyia fedha kwa njia ya hundi, hati za malipo au njia yoyote inayokubalika na benki
 • Akaunti ya kukusanyia fedha imeunganishwa na huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ili kukuwezesha kudhibiti fedha yako kikamilifu

Pata fursa ya kuunganishwa na huduma za dirisha la malipo ya kibenki mahala ulipo na uiache benki ikufuate

Inaboresha ukusanyaji wa fedha na inaokoa muda wa wateja wako. Unganishwa na huduma ya Dirisha la upokeaji fedha na hundi za malipo kutoka kwa wateja wako kwa niaba yako. Dirisha hili litakuwa ndani ya eneo ambalo biashara yako ipo. Ni njia nzuri inayookoa muda na nisalama.

Ninaombaje Huduma ya NBC ya Mhudumu Anayetembelea Wateja

Jaza fomu yetu mtandaoni nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea Tawi la NBC lililopo jirani

Manufaa ya Mhudumu wa NBC Anayetembelea Wateja
 • Huboresha ukusanyaji wa fedha
 • Inakupunguzia usimamizi wa ndani
 • Inapunguza mlolongo wa kufanya hesabu
 • Inapunguza athari za usalama wa fedha zako
Taarifa muhimu
 • Mhudumu maalum atakuwa kwenye eneo lako
 • Mhudumu atachukua fedha taslimu na kukupatia stakabadhi
 • Tunasafirisha fedha yako na kukuwekea kwenye akaunti yako

Kwa nini upoteze siku na muda wako, wakati tunaweza kukuhudumia?

Kitengo chetu cha Huduma ya Kusafirisha Vifurushi inakupatia wakala wa kusafirisha na kukusanya nyaraka zako mbalimbali kama vile hundi, kadi, taarifa na zaidi. Inapatikana wakati wowote na mahali popote.

benefits - icon
Ninaombaje Huduma ya Kusafirisha Vifurushi ya NBC
 • Jaza tu fomu yetu mtandaoni na tutawasiliana na wewe, au tembelea Tawi la NBC lililopo karibu yako
benefits - icon
Manufaa kwako
 • Inapunguza gharama za uendeshaji
 • Inaokoa muda
 • Ni salama kwani nyaraka zako zitachukuliwa kutoka ofisini na mtoa huduma anayeaminika
benefits - icon
Taarifa muhimu
 • Wakala wetu atakusanya au kukuletea nyaraka kwa wakati wako
 • Wakala wetu anakusanya nyaraka kutoka kwako na kutuletea Benki
 • Wakala wetu anakusanya nyaraka kutoka Benki na kukuletea eneo la biashara yako
Professional using a laptop

Shughulikia biashara yako na sisi tutakusaidia masuala ya kiitifaki

Huduma ya kuweka fedha taslimu kupitia gari la benki

Mhudumu wetu wanakuja na kuhesabu fedha pale ulipo, anazisafirisha na kuweka kwenye akaunti yako. Mhudumu huyu pia anaweza kuchukua fedha kwa niaba yako kutoka kwenye akaunti yako, kuisafirisha na kuifikisha eneo lako la biashara.

Huduma ya kusafirisha Fedha bila mhudumu wa benki

Tunakusanya fedha kutoka ulipo na kuifikisha kwa mhudumu wa benki ambaye ataihesabu na kuiweka kwenye akaunti yako. Pia tunasafirisha na kukuletea fedha taslimu pale ulipo na mhudumu wako atazipokea na kuzihesabu.

benefits - icon
Ninaombaje Huduma ya NBC ya Kuweka Fedha Popote ulipo
 • Jaza tu fomu yetu mtandaoni na tutawasiliana na wewe, au tembelea Tawi la NBC lililopo karibu yako
benefits - icon
Manufaa
 • Kuchukua fedha taslimu kwa wakati wako
 • Fedha zitawekwa kwenye akaunti yako kwa wakati
 • Unaendelea na biashara yako na kutuachia sisi masuala ya kusimamia fedha yako
 • Unaongeza usalama kwenye huduma za kibenki
 • Unakuwa salama dhidi ya hatari zinazohusiana na kushughulikia fedha taslimu wakati wa kusafirisha na wakati wa kupokea risiti ya kuthibitisha kuweka
benefits - icon
Taarifa muhimu
 • Njia salama kabisa ya kusafirisha fedha yako kutoka ulipo kwenda kwenye matawi ya benki yetu na kutoka matawini hadi ulipo

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191

Tuandikie baruapepe:

nbc_corporateservices@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi