Wakati ambapo shirika lako linakua, huduma hizi zitakuwezesha kuweka sawa matumizi yako ya huduma za kibenki.

 

NBC Ltd itatumia na kutoa taarifa zako binafsi pale tu inapohitajika ili kukupa huduma ulizoomba au unazohitaji kutoka NBC. Angalia Sera ya Utunzaji Taarifa ya NBC.

 

card with cash
Fanya miamala bila mipaka

Tumia akaunti yako kwa njia ya Mtandao muda wowote na popote.

Glob icon
Lipa watu wengi mara moja

Lipa moja kwa moja kwa mkupuo kutoka kwenye akaunti yako.

Badilishana majalada katika hali ya usalama

Programu yetu ya File Gateway huwezesha utumaji wa taarifa kati yako na Benki ya NBC kufanyika kwa usalama zaidi.

Professional using a laptop

Pangilia matumizi ya akaunti ya kampuni yako popote uwapo

Huduma zetu za kibenki za Makampuni kwa njia ya mtandao hukupa fursa ua kuendesha miamala kwa njia ya mtandao, popote pale duniani. Hii hufanya huduma za kibenki za shirika lako ziwe rahisi zaidi, nzuri na za kuaminika.

Namna ya kuanza

Wasilisha nyaraka zifuatazo unapoomba

 • Jaza fomu za maombi na uziwasilishe kwenye matawi yetu au kwa Meneja Mahusiano wako au jaza fomu hii nasi tutawasiliana nawe
Manufaa 
 • Kupata taarifa za akaunti, mfano salio na taarifa nyingine
 • Kuchakata malipo kwa njia ya mtandao, mfano malipo Kati ya Benki za Kitanzania (TISS) malipo kwenye benki za kimataifa
 • Tunakuhudumia mara moja malipo makubwa kama gawio, mishahara na malipo ya watoa huduma
 • Kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti zako nyingine za NBC
 • Kuhamisha fedha kwenye akaunti tofauti tofauti za benki za ndani kwa wakati mmoja
 • Kufanya malipo yoyote (ya nje, ya ndani, malipo ya ACH, TISS, malipo kwa wasambazaji wako, malipo ya mshahara kwa wafanyakazi wako)
 • Kufanya malipo ya moja kwa moja kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kwenye akaunti nyingine za TRA zilizoko Benki Kuu
 • Inapatikana popote na wakati wowote (ndani na nje ya nchi) ukiwa umeunganishwa kwenye intaneti
Taarifa muhimu
 • Inatumia vihakiki vya aina mbili: jina, namba ya siri na kihakiki cha kugusa ambavyo hukupatia fursa ya kufungua kwa awamu moja tu (one-time password-OTP)

Tekeleza malipo makubwa ya mkupuo popote ulipo kwa kubofya mara moja tu

Omba kujiunga na mfumo wa NBC wa Malipo Makubwa ya Mkupuo na ufurahie malipo makubwa na ya moja kwa moja kwa wateja wengi, wakiwamo malipo ya wafanyakazi wasio na akaunti za benki.

benefits - icon
Namna ya kuanza

Jaza fomu kwa njia ya mtandao na tutawasiliana na wewe, au tembele Tawi la NBC lililopo jirani yako.

benefits - icon
Manufaa
 • Njia ya moja kwa moja ya kufanya Malipo mengi kwa mara moja (Straight-Through Processing-STP)
 • Ufanisi katika kufanya malipo kwa watu wengi kwa mara moja
 • Uchukuaji wa Fedha kwa Njia ya Simu Bila Kadi
 • Malipo Makubwa ya Mkupuo kwa Njia ya Simu ya Mkononi
benefits - icon
Taarifa muhimu

Wakala Maalum wa mitandao ya simu

 • Mawakala wa makampuni ya simu, hukuwezesha kununua salio (e-Float), kutoka kwenye tawi lolote la NBC. NBC hushirikiana na makampuni ya simu kutoa huduma kwa mawakala wao wanao nunua salio kwa jumla

Jihakikishie usalama na ufanisi kwa kutumia programu ya File Gateway

Programu ya File Gateway ni njia rahisi na bora katika kutumiana majalada kati ya NBC na ofisi yako. Huduma hii inakupatia fursa ya kuweka alama za uhakiki pamoja na kuweka namba za siri ili kuimarisha usalama na usiri wa majalada yako.

benefits - icon
Namna ya kuanza
 • Jaza fomu mtandaoni na tutawasiliana na wewe, au tembelea Tawi la NBC lililopo karibu yako
benefits - icon
Manufaa
 • Njia ya kufanya malipo moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako kwenda kwa unae mtumia kwa kutumia mtandao
 • Uhakika wa usalama wa taarifa zinazo tumwa kati yako na NBC
 • Ina uwezo wa kushughulikia nyaraka ya miundo aina zote inayo kubalika na inayotumika
 • Unapata ripoti yenye taarifa za muamala mara tu baada ya kuukamilisha
benefits - icon
Taarifa muhimu

Huduma za Programu ya “File gateway” hufanya kazi za aina mbili:

Kutuma majalada ya taarifa za Akaunti:

 • Majalada hutumwa kutoka kwenye mfumo wa NBC kuja kwenye mfumo wako yakiwa na maelezo ya kina kuhusu miamala iliyofanyika kwenye akaunti yako, mfano taarifa ya kukamilika kwa malipo.

Kutuma Nyaraka za Malipo:

 • Majalada ya malipo hutumwa kutoka kwenye mfumo wako kuja NBC kwa ajili ya kushughulikia na kukamilisha malipo.

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191

Tuandikie baruapepe:

nbc_corporateservices@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi