Unapata fursa ya kuingia kwenye soko la wateja wakubwa na kuuza zaidi kwa kutumia mashine za POS zinazowekwa kwenye vituo vya mauzo. Ni njia rahisi na nzuri ya kupokea malipo kwa usalama. 

Omba

Faida za huduma za kibenki za mashirika na uwekezaji

card with cash
Mzunguko wa hela

Ina kuhakikishia usimamizi mzuri wa mzunguko wa hela zako.

Glob icon
Ugharamiaji

Ni njia nzuri ukilinganisha na mikopo ya dharura.

Ushindani

Inakuongezea fursa ya majadiliano na makubaliano.

card with cash
Majadiliano na makubaliano

Unajadiliana na kupata mkataba wa masharti nafuu kuliko washindani wako.

Glob icon
Uwezeshaji

Kuza mtaji wako kwa kupokea fedha za malipo ya awali.

Professional using a laptop

Tutakulinda dhidi ya athari zitokanazo na uagizaji au uuzaji wa bidhaa nje ya nchi

Unapokuwa na Hati ya Malipo, Athari zinazoweza kutokea kwenye malipo unakuwa umezihamishia NBC. Unaweza ukafanya majadiliano kwa utulivu na hata kuomba kupunguziwa bei na wanaokuuzia au kuomba kusogezewa muda wa kulipa ili kusubiri mzunguko wako wa fedha utengemae.

Hati ya Malipo ya Kuingiza Bidhaa Hati ya Malipo ya Kuuza Nje Bidhaa

Haya ni makubaliano thabiti yanayofanywa na Benki ya NBC kama ‘Benki yenye Dhamana ya Kulipa’ unapoiomba imlipe mnufaika au msambazaji wako baada ya kuwasilisha nyaraka za madai.


Manufaa

 • Inadumisha udhibiti wa usalama wa miamala
 • Hati ya Malipo haitenguliwi, hivyo hakuna masharti wala vigezo (kama vile tarehe ya mwisho ya kutuma mzigo, masharti ya malipo na masharti mengine yaliyoandikwa kwenye nayaraka) vinavyoweza kubadilika isipokuwa kwa makubaliano na Benki Iliyotoa Hati, Benki Iliyothibitisha (kama ipo) na mhusika mkuu kabla haijapitiwa upya

Mwombaji au mnunuzi (mteja wako) anakupatia Hati ya Malipo kutoka kwenye benki yake kuja kwako kupitia NBC (kama benki inayokushauri) na itahakikiwa usahihi wake. Kama itaonekana sahihi, tutakushauri hatua za kuchukua.

Manufaa

 • Unakuwa na uhakika wa malipo yako kutoka kwa mnunuzi au wateja utakapowasilisha nyaraka za madai yako

Tuachie tukusaidie kuboresha mzunguko wa fedha zako

Kwa kuwa na Hatifungani/Dhamana ya NBC una uhakika wa kulipwa hata kama muuzaji au mnunuzi wako atashindwa kutimiza masharti ya mkataba. Benki ya NBC ina aina mbalimbali za dhamana ambazo zinatumika kulipa inapotokea mtu mwingine anashindwa kukulipa. 

benefits - icon
Benki ya NBC aina mbalimbali za Hatifungani/Dhamana, ikiwamo:
 • Hatifungani/Dhamana ya Zabuni
 • Dhamana ya Utendaji
 • Dhamana ya Malipo ya Awali
 • Dhamana za Kusafirisha
 • Hatifungani za Bandari
 • Dhamana ya malipo
 • Dhamana na Kukaa na Mzigo, nk.

Pokea na kufanya malipo ya ndani na nje kwa usalama zaidi

Jihakikishie usalama wa malipo yako na udhibiti mzuri wa bidhaa zinazotumwa kupitia huduma ya gharama ya kusafirishia kuja na kwenda nje.

Nyaraka za ukusanyaji malipo ya Kuingiza Bidhaa Nyaraka za Malipo ya Kusafirisha Nje kwa ajili ya Ukusanyaji

Nyaraka za Malipo ya NBC kwa ajili ya Ukusanyaji ni njia salama na ya uhakika ya kupata bidhaa kutoka popote duniani.

Kwa kuwa nyaraka hutunzwa na benki, unaweza:

 • Kufanya majadiliano na kupata kwa masharti nafuu (Mfano, kulipia baada ya siku 30)
 • Unalipia tu wakati bidhaa zako zimeshapakiwa kwa ajili ya kusafirishwa

Pokea bidhaa unazosafirisha kwa kuwa tu na waraka wa malipo ya kusafirisha nje. Tunahakikisha kwamba wanunuaji wanapokea bidhaa zao baada ya nyaraka zao kuwa zimetolewa na benki zao.

Ukusanyaji wa nyaraka ni salama zaidi katika kufanya malipo kuliko kuwa na akaunti ya biashara kwa sababu:

 • Miamala yote hufanyika kwenye chaneli za benki
 • Nyaraka hutolewa baada ya kupokea maelekezo
Professional using a laptop

Inakusaidia kutimiza Majukumu yako ya malipo kwaajili ya uingizaji au usafirishaji wa bidhaa

Inakusaidia kudhibiti athari zitokanazo na ununuzi wa bidhaa, unapata wasaa wa kufanya majadiliano kuhusu masharti ya mkopo na inakupunguzia msongo kuhusu mzunguko wa fedha zako kama utatumia bidhaa yoyote ya NBC ya Ufadhili wa Biashara.

benefits - icon
Mkopo wa Baada ya Kuingiza Bidhaa

Huu ni mkopo wa muda wa mfupi (muda uliobainishwa) unaokusaidia kutimiza masharti ya kulipia bidhaa.

Manufaa

 • Unasaidia kuboresha mzunguko wa fedha
 • Una rasilimali fedha inayo patikana kwa wingi ili kukusaidia kulipia gharama za bandari/viwanja vya ndege, kuhifadhi na kuuza
 • Kuwalipa wasambazaji wako wanapowasilisha bidhaa kwako au muda wa kulipia unapofika
benefits - icon
Huduma za kulipia kwa Ankara-Kuingiza Bidhaa

Tafuta fedha kwa muda mfupi kwa kutumia ankara za biashara na nyaraka za kusafirishia bidhaa kupitia kwenye miamala benki.

Manufaa

 • Mzunguko mzuri wa fedha
 • Inapunguza gharama ikilinganishwa na mikopo ya dharura
 • Kumlipa msambazaji anapokuletea tu bidhaa au muda wa mkataba unapofika
benefits - icon
Huduma ya Malipo ya Ankara kifani

Haya ni malipo ya awali kwa muuzaji yanayofanyika kabla bidhaa hazijatumwa.

Manufaa

 • Hukusaidia kuuboresha mzunguko wa fedha
 • Inapunguza muda wa uhakiki wa miamala
benefits - icon
Huduma ya Malipo Kabla ya Bidhaa Kutumwa

Hii ni fedha inayotumwa kwa muuzaji (kwa mujibu wa muda maalum) kwa kuzingatia ama mkataba wa mauzo, hati ya manunuzi au Hati ya Mkopo.

Manufaa

 • Kupata fedha mapema
 • Ina gharama nafuu za kuwezeshwa kuliko mkopo wa dharura
 • Inakupa wigo pana wa kujadiliana kuhusu masharti ya mkataba
 • Inapatikana kwa fedha za ndani na za kigeni

 

benefits - icon
Ankara ya Punguzo la Bei

Huduma hii hutumika unapokuwa unauza bidhaa zako moja kwa moja pasipo kuhusisha Benki. NBC inakupa fursa ya kuingia nayo mkataba maalum ili ilipie deni kwa niaba yako endapo muda wa kufanya malipo umefika na hauja fanikisha.

Manufaa

 • Unapata fedha ndani ya muda mfupi kwa kutumia ankara za biashara na nyaraka za kusafirishia bidhaa husika
 • Inapatikana kwa biashara za ndani na za nje
benefits - icon
Punguzo kwenye Hatifungani za Kuuza Nje

Inakuwezesha kupata fedha mapema.

Faida

 • Inaboresha mzunguko wa fedha
 • Inarahisisha biashara yako

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191

Tuandikie baruapepe:

nbc_corporateservices@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi