Jua namna rahisi ya kutuma fedha kwa mtu, hata kama hawana akaunti ya benki. Unaweza pia kukomboa muamala wa kutuma fedha bila kadi na pia unaweza kuweka fedha wakati wowote.

Jinsi ya kutuma fedha taslimu

Tunakuonesha jinsi ya kutuma fedha kwa mtu, hata akiwa hana akaunti ya benki.

Fahamu zaidi

 

Jinsi ya kukomboa vocha ya pesa

Hatua za haraka na rahisi za kutoa pesa kwenye ATM bila kuhitaji kuingiza kadi.

Fahamu zaidi

 

Jinsi ya kuweka fedha

Tazama jinsi ilivyo rahisi kuweka fedha kwenye ATM wakati wowote.

Fahamu zaidi

Jinsi ya Kutuma fedha
 • Jinsi ya kutuma fedha kutoka kwenye ATM

  1. Ingiza kadi yako na weka neno la siri
  2. Chagua ''Huduma Nyingine''
  3. Chagua "Vocha ya Pesa"
  4. Ingiza Thamani ya Vocha Unayonunua (katika mafungu ya 5000)
  5. Unda Namba ya Siri yenye tarakimu 4 kwa ajili ya mpokeaji na Thibitisha
  6. Ingiza namba ya simu ya mpokeaji
  7. Thibitisha Muamala
  8. Kitambulisho cha vocha za pesa huonyeshwa na risiti huchapishwa
  9. Tuma PIN yenye tarakimu 4 na kitambulisho cha vocha kwa mpokeaji kudai fedha
Jinsi ya kutoa pesa iliyotumwa
 • Jinsi ya kukomboa vocha ya pesa kwenye ATM

  1. Chagua "Huduma Bila Kadi"
  2. Ingiza kitambulisho cha vocha ya pesa na Namba ya Siri  iliotolewa na Mtumaji
  3. Ingiza Kiasi Halisi cha Fedha kilichotumwa na Mtumaji
  4. Thibitisha Muamala, ATM itatoa Kiasi cha vocha
Namna ya kuweka fedha
 • Namna ya kuweka fedha

  1. Ingiza Kadi yako ya Malipo na Uweke Namba ya Siri yako kwenye ATM yoyote ya NBC
  2. Chagua 'Kuweka Fedha'
  3. Ingiza noti zako kwenye amana ya fedha (hadi noti 40 kwa kwenda)
  4. Bonyeza 'Imefanyika' ili kumaliza Muamala wako au 'Ongeza zaidi' kwa amana ya zaidi
  5. Thibitisha amana na kusanya risiti yako ya amana

Je, unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC