Jua jinsi ilivyo rahisi kujisajili na kutumia NBC Kiganjani kuhamisha fedha, kununua umeme na zaidi.

Tuma pesa na hamisha fedha

Tunakuonesha hatua chache rahisi za jinsi ya kutuma pesa au kuhamisha fedha kwenda akaunti nyingine au kwenda kwenye mtandao wa simu kwa kutumia NBC Kiganjani.

Fahamu zaidi

 

Jinsi ya kuongeza mnufaika

Hatua za haraka na rahisi za kuongeza mnufaika wa muda wa maongezi, uhamishaji fedha, ununuzi wa umeme.

Fahamu zaidi

 

Nunua Umeme na jaza muda wa Maongezi

Tazama jinsi ilivyo rahisi kununua umeme au kuongeza muda wa maongezi bila kutoka nyumbani au ofisini kwako.

Fahamu zaidi

Kuomba taarifa za miamala na kubadili Neno la siri (PIN)

Mwongozo rahisi unaokuonesha namna ya kupakua taarifa za miamala pamoja na kubadili neno lako la siri (PIN).

Fahamu zaidi

Jinsi ya kutuma au kuhamisha fedha
 • Jinsi ya Kutuma fedha taslimu

  1. Piga *150*55#  na Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 4 Toa / Tuma pesa - Cash Popote
  3. Ingiza namba ya simu ya mpokeaji
  4. Ingiza kiasi cha pesa katika mafungu ya 5000
  5. Chagua Akaunti unayotaka kuhamisha fedha kutoka
  6. Ingiza namba ya siri yoyote yenye tarakimu 4 kwa ajili ya mpokeaji
  7. Thibitisha Namba ya Siri. Tuma Namba ya Siri kwa Mpokeaji
  8. Thibitisha Muamala, Pokea ujumbe wa Uthibitisho wa Muamala. SMS Itatumwa kwa Namba ya Mpokeaji yenye Maelezo ya Vocha.
  9. Tuma PIN kwa Njia Tofauti kwa Mpokeaji kwa Sababu za Ki usalama
 • Jinsi ya kuhamisha fedha kwenda akaunti ya NBC

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 1 Tuma Pesa
  3. Chagua 2 Akaunti Nyingine NBC
  4. Weka namba ya Akaunti ya Mpokeaji
  5. Weka kiasi cha Kutuma 
  6. Chagua Akaunti ya kutoa fedha
  7. Bonyeza 1 Kuthibitisha
  8. Screen ya Uthibitisho na SMS
 • Jinsi ya kuhamisha fedha kwenda mtandao wa Simu

  1. Piga *150*55# na Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 1 Tuma Pesa
  3. Chagua 3  Mitandao ya Simu
  4. Chagua Mtandao wa simu wa kutuma pesa kwa (Airtel Money,MPESA,Tigopesa,Ezypesa)
  5. Chagua namba unayoitumia fedha (namba yako au namba nyingine)
  6. Ingiza namba unayotaka kutuma pesa kwa
  7. Ingiza kiasi unachotaka kuhamisha
  8. Chagua akaunti ya kutoa fedha
  9. Thibitisha Muamala
Jinsi ya kuongeza mnufaika
 • Jaza muda wa maongezi

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 8 Lugha/Akaunti yangu
  3. Chagua 2 Ongeza/Badili Mnufaika
  4. Chagua 3 Mitandao-Muda wa Maongezi
  5. Chagua 1 Mnufaika mpya
  6. Chagua Mtandao ( wasiliana na mpokeaji kama huna uhakika)
  7. Ingiza namba ya simu
  8. Ingiza jina la utani la mnufaika (zisizidi herufi 15)
  9. Bonyeza 1 kuthibitisha
  10. Screen ya Uthibitisho
 • Uhamisho wa fedha kwenda akaunti ya NBC

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 8 Lugha/Akaunti yangu
  3. Chagua 2 Ongeza/Badili Mnufaika
  4. Chagua Akaunti za Benki - NBC
  5. Chagua 1 Sajili Mnufaika
  6. Chagua 1 Akaunti nyingine ya NBC
  7. Weka namba ya Akaunti ya Mpokeaji
  8. Ingiza Jina la Utani la Mnufaika
  9. Bongeza 1 kuthibitisha
  10. Screen ya Uthibitisho
 • Umeme

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 8 Lugha/Akaunti yangu
  3. Chagua 2 Ongeza/Badili Mnufaika
  4. Chagua 2 Kampuni zilizohifadhiwa
  5. Chagua 1 Sajili Kampuni
  6. Chagua 3 LUKU
  7. Weka namba ya Mita 
  8. Ingiza Jina la utani la kampuni
  9. Bonyeza 1 kuthibitisha
  10. Screen ya Uthibitisho
Jinsi ya Kununua umeme na kuongeza Muda wa maongezi
 • Nunua umeme

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 2 Lipa Bili
  3. Chagua 1 Chagua Kampuni
  4. Chagua 3 Prepaid Electricity
  5. Chagua 1 LUKU
  6. Weka namba ya mita
  7. Ingiza kiasi
  8. Chagua Akaunti ya Kutoa fedha  
  9. Bonyeza 1 kuthibitisha
  10. Screen ya Uthibitisho
  11. Pokea tokeni kupitia SMS
 • Jaza muda wa maongezi

  Nambari yako mwenyewe:

  1. Piga *150*55# na Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 3 Muda wa Maongezi
  3. Chagua 1 Mtandao
  4. Chagua Mtandao wa kununua Muda wa Maongezi (Airtel/Vodacom/Tigo/Zantel/TTCL Prepaid)
  5. Chagua 1 Namba yako
  6. Ingiza kiasi
  7. Chagua akaunti ya kutoa fedha
  8. Thibitisha MuamalaOther number

  Nambari nyingine

  1. Piga*150*55# and Ingiza Namba ya Siri
  2. Chagua 3 Muda wa Maongezi
  3. Chagua 1 Mtandao
  4. Chagua Mtandao wa kununua Muda wa Maongezi (Airtel/Vodacom/Tigo/Zantel/TTCL Prepaid) 
  5. Chagua 2 Namba nyingine
  6. Ingiza namba ya simu
  7. Ingiza kiasi
  8. Chagua Akaunti ya kutoa fedha
  9. Thibitisha muamala
Jinsi ya kuomba taarifa za kibenki na kubadili Neno lako la siri (PIN)
 • Omba taarifa za miamala

  1. Piga *150*55# na Ingiza namba ya siri
  2. Chagua 6 Huduma Nyingine
  3. Chagua 3 Maombi
  4. Chagua 2 Taarifa ya Akaunti
  5. Chagua Akaunti namba
  6. Uthibitisho wa Screen (ombi lako limekubaliwa na utapokea taarifa yako katika siku 3 za kazi)
 • Badilisha neno lako la siri (PIN)

  1. Piga *150*55# 
  2. Bonyeza 1 kama hukumbuki namba yako ya siri
  3. Tafadhali kaa karibu na debit kadi yako wakati wa kubadili neno la siri . Bonyeza 1 kuendelea
  4. Ingiza namba ya Akaunti
  5. Weka herufi ya 2nd na 3rd  ya namba ya mwaka wa kuzaliwa YYYYMMDD
  6. Ingiza tarakimu ya 7th, 9th, 10th, 15 th ya debit kadi namba  (kwa kutumia kadi yako)
  7. Bonyeza 1 kuthibitisha
  8. Screen ya Uthibitisho na SMS

Je, unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC