Tambua jinsi ilivyo rahisi kujisajili kupata huduma za kibenki mtandaoni na utumie njia hiyo kuhamisha fedha, kununua umeme na zaidi.

Jisajili huduma za kibenki mtandaoni

Tunakuonesha kwa hatua chache na rahisi Jinsi ya kujisajili na benki ya Mtandaoni.

Fahamu zaidi

 

Jinsi ya kuhamisha fedha

Hatua za haraka na rahisi za kuhamisha fedha kwenda Akaunti nyingine au kwenda Mitandao ya Simu.

Fahamu zaidi

 

Jinsi ya kunua umeme

Tazama jinsi ilivyo rahisi kununua Umeme bila kutoka nyumbani kwako au ofisini.

Fahamu zaidi

Pata taarifa za miamala

Mwongozo rahisi unaokuonesha namna ya kupakua taarifa za kibenki kwenye akaunti yako.

 

Fahamu zaidi

Jinsi ya kujisajili
 • Usajili binafsi

  1. Tembelea www.nbc.co.tz
  2. Bonyeza Kuingia karibu na kichupo cha Utaftaji
  3. Bonyeza kujisajili Kwenye Chaguo la kuingia kwa Binafsi
  4. Ingiza Taarifa zako Kisha kubaliana na Vigezo na Masharti
  5. Utapokea Namba ya siri ya kutumika mara moja Kupitia Ujumbe wa Simu
  6. Ingiza Namba ya siri kisha Bonyeza Kifuatacho
  7. Unda Jina la Mtumiaji na Neno la Siri kwenye Screen ya Uthibitisho wa Neno la Siri
  8. Bonyeza Kifuatacho
  9. Screen ya Uthibitisho
Jinsi ya kuhamisha fedha
 • Kwenda akaunti nyingine

  1. Tembelea www.nbc.co.tz
  2. Bonyeza Kuingia karibu na kichupo cha Utaftaji
  3. Bonyeza Kuingia kwenye Chaguo la Kuingia kwa Binafsi 
  4. Ingiza Jina la Mtumiaji na Neno la Siri na Bonyeza kitufe cha Kuingia
  5. Chagua  'uhamishaji na malipo' 
  6. Chagua Akaunti unayotaka kuhamisha fedha kutoka na Mlipwaji au Akaunti unayotaka kuhamisha fedha kwa
  7. Kwa Mlipwaji aliyesajiliwa, Ingiza Kiasi, maelezo ya malipo na Bofya Kifuatacho (Kwa Mlipwaji Mpya, Ingiza maelezo ya mteja na Ufuate hatua Zifuatazo)
  8. Hakiki na Uthibitishe Maelezo ya Muamala
  9. Screen ya Uthibitisho
 • Kwenda mtandao wa simu

  1. Tembelea www.nbc.co.tz
  2. Bonyeza Kuingia karibu na kichupo cha Utaftaji
  3. Bonyeza Kuingia kwenye kichupo cha Kuingia kwa Binafsi
  4. Ingiza Jina la Mtumiaji na Neno la Siri na Bonyeza Kuingia
  5. Chagua ' Uhamishaji na ' Malipo '
  6. Chagua ' Lipa Bili za Matumizi yangu' kwenye kona ya kulia ya screen
  7. Chagua Mlipwaji, Bonyeza Kifuatacho na Ingiza Kiasi (Kwa Kampuni iliosajiliwa)
  8. Kwa Mlipwaji Mpya, Chagua  Wallet ya Simu chini ya Aina ya Kampuni na Chagua kampuni
  9. Ingiza Namba ya Simu
  10. Ingiza Kiasi
  11. Ongeza kwenye Orodha ya Mlipwaji kama ukitaka
  12. Bonyeza Kifuatacho
  13. Thibitisha Maelezo na Bonyeza kifuatacho
  14. Ikiwa uhamisho umefanywa kwa Mlipwaji aliepo, muamala utakuwa na mafanikio
  15. Ikiwa uhamisho umefanywa kwa Mlipwaji mpya, OTP itatumwa kwa Mteja ili kuhalalisha kisha muamala utakuwa na mafanikio
Jinsi ya kununua umeme
 • Nunua umeme

  1. Tembelea www.nbc.co.tz
  2. Bonyeza Kuingia karibu na kichupo cha Utaftaji
  3. Bonyeza Kuingia kwenye kichupo cha Kuingia kwa Binafsi
  4. Ingiza Jina la Mtumiaji na Neno la Siri na Bonyeza kitufe cha Kuingia
  5. Chagua  'Uhamishaji na Malipo'
  6. Chagua 'Lipa Bili za Matumizi yangu' kwenye kona ya kulia ya screen
  7. Chagua Mlipwaji, Bonyeza Kifuatacho na Uingize kiasi (Kwa Kampuni iliohifadhiwa)
  8. Kwa Mlipwaji mpya, Chagua Umeme wa kulipia kabla Kwenye Aina ya Mtoa Huduma na uchague LUKU
  9. Ingiza namba ya Mita na Bonyeza Kifuatacho
  10. Ingiza Kiasi na Bonyeza Kifuatacho
  11. Hakiki na Uthibitishe Maelezo ya Muamala
  12. Screen ya Uthibitisho
Jinsi ya kuomba taarifa za miamala
 • Omba taarifa za miamala

  1. Tembelea www.nbc.co.tz
  2. Bonyeza Kuingia karibu na kichupo cha Utaftaji
  3. Bonyeza Kuingia kwenye kichupo cha Kuingia kwa Binafsi
  4. Ingiza jina la Mtumiaji na Neno la Siri na Bonyeza kuingia
  5. Chagua Akaunti na Miamala
  6. Chagua Akaunti Namba
  7. Chagua Taarifa za kichupo
  8. Pakua taarifa

Je, unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC