Kama unaweza kupata intaneti, unaweza kufanya miamala yako mingi ya kibenki bila kulazimika kutembelea tawi lolote la NBC. Jisajili na huduma za NBC Online Banking na ufurahie kufanya miamala popote na wakati wowote unapohitaji.

Inafanyaje kazi

hand with a tick - icon
NBC Online Banking inakuwezesha:
 • Kuangalia salio la akaunti yako
 • Kupata taarifa za akaunti yako
 • Kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti zako nyingine
 • Kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti za benki nyingine nchini
 • Kununua muda wa maongezi wa simu za mitandao yote nchini
 • Kulipia bili mbalimbali za LUKU, ving’amuzi, usafiri wa ndege na nyingine nyingi
 • Kuhamishia fedha kwenda kwenye simu yako ya mkononi kama vile Mpesa, TigoPesa, AirtelMoney, nk
 • Kuhifadhi majina ya watu au bili unazolipia mara kwa mara
 • Kuomba kitabu cha hundi
 • Kuweka utaratibu wa kuhamisha fedha kielektroniki hasa unapokuwa na malipo ya kufanya kila mwezi kutoka kwenye akaunti yako ya NBC kwenda kwenye akaunti husika. Inaweza kuwa kulipia huduma mbalimbali za kila mwezi
laptop and mouse icon
Kujiunga na Huduma za NBC Online Banking?
 • Pakua Fomu hii,  ijaze na kuipeleka kwenye tawi lolote la NBC lililopo karibu nawe ili isaniwe (utatakiwa uwe na kitambulisho chako)
 • Ukishajiunga pakua program ya NBC Online Banking kutoka Playstore au App Store kisha uanze kutumia kwa kufuata maelezo rahisi kabisa
 • Huduma hii ni kwa wote ambao tayari ni wateja wa NBC
apply icon
Ni salama kiasi gani?

Ni salama kwa sababu:

 • Utapewa jina maalum na namba ya siri ambapo bila hiyo akaunti yako haiwezi kutumika
 • Kila mara unapohitaji kutumia huduma ya NBC Online Banking, NBC itakutumia namba ya siri ya kutumika mara moja

Zilinde fedha na akaunti yako kwa kufanya yafuatayo:

 • Hakikisha unatunza kwa usiri mkubwa jina na namba yako ya siri wakati wote
 • Usihifadhi namba yako ya siri kwenye simu yako
 • Daima funga kabisa kurasa za Huduma NBC Online Banking baada ya kuitumia na kabla hujatembelea tovuti nyingine au unapotoka na kuacha kompyuta au simu yako bila usalama
 • Angalia mara ya mwisho uliingia lini na ukihisi kulikuwa na jaribio lolote la kuingia kwenye akaunti yako tujulishe haraka
 • Hakiki mara kwa mara salio la akaunti yako na miamala uliyowahi kufanya

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?

Wasiliana nasi:

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie:

NBC_Digital.Channels@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTawi la NBC