Kupitia uzoefu wa miaka zaidi ya 20, NBC inakupatia aina mbalimbali za bima kwa ajili ya watu wako na mali zako.

bank notes - icon
Ushauri wa Kitaalam

Tuna uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye masuala ya bima.

A family potrait - icon
Uhuru wa Kuchagua

Unachagua bima inayoendana na mahitaji na uwezo yako.

A family potrait - icon
Madai ya Fidia

Kasi na usahihi ni lugha yetu katika kukulipa fidia zako za bima. Jaza tu fomu ya madai kisha uilete tawini

 

Couple in a car

Bima nafuu kwa ajili ya gari lako

NBC inakupa uchaguzi wa bima ya gari inayokidhi mahitaji yako na kwa bei nafuu dhidi ya ajali, uharibifu, wizi na madai kutoka kwa wengine.

 

bank notes - icon
Bima Kamili

Hii ni bima kwa ajili ya gari lako likiibiwa, likiungua moto au likipata ajali na kama mtu mwingine atakuwa anakudai kwa kumgonga au kumharibia gari lake.

A family potrait - icon
Bima kwa ajili ya mtu mwingine, moto au wizi

Bima kwa ajili ya wizi, moto, uharibifu na madai ya mtu mwingine (pale ambapo ajali imetokana na makosa yako).

A tick - icon
Bima kwa ajili ya mtu mwingine

Hii ni bima kwa ajili ya madai ya mtu mwingine pale ambapo umegongana na gari lingine na wewe ndiye mwenye makosa.

Couple in a car

Kata bima NBC kwa ajili ya nyumba yako na vitu vya nyumbani kwako

Bima kwa ajili ya nyumba yako kuanzia kwenye sakafu hadi paa, nje na ndani, inayojumuisha vitu vya thamani vya nyumbani kwako.

Manufaa ya Bima ya Nyumba ya NBC

Ni bima kwa ajili ya:

 • Uharibifu wa jengo
 • Uharibifu wa samani mbalimbali zilizopo nyumbani kwako
 • Upotevu unaotokana na moto au ujambazi
 • Uharibifu au upotevu wa vitu vya ndani

Pia inahusisha:

 • Bima ya Madeni

Ilinde familia yako kwa kukata Bima ya Maisha NBC

Katia bima samani za ndani ya nyumba yako dhidi ya hatari zozote. NBC Tunatoa bima za kifo, kupunguzwa kazini na ulemavu wa kudumu utokanao na ajali.

Tutakusaidia kuwa na bima kwa ajili ya familia yako

Kupitia huduma mbalimbali za bima zinazoambatanishwa na akaunti na mikopo ya NBC, zinakuwezesha kuishi kwa amani na furaha ukijua kwamba mkopo wako una bima itakayoilinda familia yako kama kutatokea lolote.

 • Faida za Bima iliyoambataniswha na akaunti za NBC

  bank notes - icon
  Bima ya Mazishi kwa Akaunti ya Akiba ya Kawaida

  Bima hii hutolewa kama mkono wa pole kwa familia za wateja wetu wote wa NBC wenye Akaunti ya Akiba ya Kawaida endapo mteja atafikwa na kifo.

  A family potrait - icon
  Bima ya Mazishi ya Takaful kwenye Huduma za Kibenki za Kiislamu

  Bima hii hutolewa kama mkono wa pole kwa familia za wateja wa NBC wenye Akaunti za Akiba za La Riba pale endapo mteja atapofariki.

  A tick - icon
  Bima ya Ajali na Mazishi kwa ajili ya Akaunti za NBC Direct

  Bima hii hutolewa kwa wateja wote wa NBC wenye Akaunti ya NBC Direct endapo watapata ajali, kifo au wakipata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

  A family potrait - icon
  Bima ya NBC ya Ajali na Mazishi wateja wa NBC Private Banking na wa NBC Privilege Banking

  Hii hutolewa kwa wateja wote wa NBC wenye akaunti za NBC Private Banking and NBC Privilege Banking endapo watapatwa na kifo au ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

  bank notes - icon
  Bima ya Mkopo

  Hii hutolewa kwa wateja wote wa NBC wenye mikopo NBC ikiwepo mkopo binafsi, overdraft, mkopo wa muda maalum na mkopo wa nyumba ili kuwasaidia kulipa kiasi cha mkopo kilichosalia kama kitatokea kifo cha ghafla au ulemavu wa maisha.

  A family potrait - icon
  Bima ya Kupunguzwa Kazi

  Ni bima ya malipo ya mkopo pale inapotokea kwamba wewe mteja mwenye mkopo umepunguzwa kazi na hujapata kazi nyingine kwa zaidi ya siku 30 mfululizo.

  A tick - icon
  Bima ya Kinga ya Mali

  Inakusaidia pale inapotokea kwamba mteja wa NBC mwenye mkopo huu amekosa ajira kwa kipindi cha zaidi ya siku 30 mfululizo. Bima itaulipia mkopo kwa niaba ya mteja kwa kipindi kisichozidi miezi tisa.

  A family potrait - icon
  Mortgage Protection Scheme

  Cover in the event of the life insured being unemployed for a period of more than 30 continuous days. The insurer will pay the loan instalments on behalf of the borrower for a maximum of nine months.

 • Bima ya Elimu

  Hakikisha watoto wako wanapata elimu bora wanayostahili. Bima ya Elimu inakusaidia kuwekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wako.

  Ninapataje Bima ya Elimu?

  Hand holding plus sign icon
  Namna ya Kukata Bima ya Elimu

  Jaza Fomu ya Bima nasi tutawasiliana nawe, au tembelea tawi la NBC lililopo karibu nawe.

  Utahitajika kuleta nyaraka zifuatazo:

  • Barua iliyosainiwa na kupigwa muhuri kutoka kwa mwenyekiti wa kata
  • Barua ya maombi ikiwa na picha yako ndogo ya rangi
  • Nakala ya kitambulisho kimojawapo kati ya hivi vifuatavyo:
   • Leseni ya udereva
   • Kitambulisho cha Taifa
   • Kitambulisho cha Mpiga Kura
   • Pasi ya Kusafiria
  Information - icon
  Kwa kukata bima ya Elimu NBC, utanufaika na yafuatayo:
  • Ni njia bora ya kuwekeza sasa kwa ajili ya elimu ya watoto wako kwa siku za baadae
  • Inajumuisha bima ya maisha na ulemavu – lolote litakalotokea kwako, elimu ya watoto wako itakuwa salama
  • Inakusaidia kukusanya fedha kwa ajili ya elimu
  • Inakupa uhuru wa kuchagua aina ya Bima ya Elimu unayotaka
  • Inakuruhusu kuchukua fedha kidogo kidogo kila mara unapohitaji
  • Kama utasitisha bima hii kabla ya muda, utalipwa fedha yako yote bila kutozwa faini yoyote
  • Ikitokea kwamba mmoja wa watoto uliowawekea bima akafariki, unaweza kuomba kurejeshewa mafao yote na kama utarejeshewa, mkataba utakuwa umeishia hapo
  Checklist - icon
  Taarifa muhimu
  • Unatakiwa uwe na umri wa kati ya miaka 18 na 60
  • Muda wa bima ya Elimu ni kuanzia miaka 7 hadi 18

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie

+255 76 898 4000 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 | 0800711177 (free) 

Tuandikie baruapepe:

NBC_Insurance@nbc.co.tz

Kata bimaTawi la NBC