Akaunti ya Kawaida ni akaunti iliyoandaliwa kwa ajili ya kukurahisishia usimamizi wa fedha zako. Unaweza kuweka na kutoa fedha katika tawi lolote la NBC au kwenye ATM, kulipia gharama na bili kupitia huduma za NBC Online Banking.

 

Ninawezaje kufungua Akaunti ya Kawaida ya Hundi NBC?

Hand holding plus sign icon
Namna ya kuanza

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lililopo karibu nawe.

Tafadhali uje na nyaraka zifuatazo wakati ili kufungua akaunti hii

 • Picha mbili ndogo za rangi
 • Kitambulisho chako – mojawapo ya hizi zifuatazo:
  • Pasi ya kusafiria
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha Taifa
  • Kitambulisho cha mpiga kura
 • Uthibitisho wa anuani ya makazi – mojawapo ya nyaraka zifuatazo:
  • Risiti ya malipo ya bili – umeme au maji  (iliyolipwa ndani ya miezi sita) inayoonesha anuani ya makazi yako
  • Barua rasmi kutoka kwa afisa mtendaji wa serikali za mitaa
  • Barua ya mwanasheria ikiainisha wazi makazi yako
 • Wasio Raia wa Tanzania watatakiwa kuleta Pasi ya kusafiri, kibali cha makazi au cha kazi
Hand holding plus sign icon
Manufaa ya Akaunti ya Kawaida ya Hundi ni:
 • Inakuwezesha kutoa fedha mara nyingi kwenye matawi ya NBC na ATM BURE
 • Inakuwezesha kuweka fedha mara nyingi kupitia matawi ya NBC na ATM BURE
 • Unapata kadi ya benki BURE
 • Unapata huduma za  NBC Online Banking na NBC Mobile Banking
 • Kuweka hati za malipo kwenda kwenye akaunti nyingine za NBC BURE

Unahitaji maelezo au msaada zaidi?


Wasiliana nasi:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191 | 0800711177 (free)

Tuanidikie:

NBCRetailProductteam@nbc.co.tz

Wasiliana nasi Tawi la NBC