Jielekeze katika kukuza biashara yako na utuachie sisi tuzunguke kukukusanyia fedha zako. Huduma zetu za Ukusanyaji wa Fedha zinakusaidia kutoa na kupeleka fedha benki au kwa mtoa huduma wako kwa haraka na kwa usalama na kwa gharama nafuu.

 

Professional using a laptop

Uzoefu mzuri wa kukusanya fedha kupitia matawi yetu huwezi kuulinganisha na mwingine

Kusanya fedha zako kupita kwenye matawi yetu zaidi ya 50 nchini.

Ninajiungaje na Huduma za Ukusanyaji Fedha kupitia Matawi ya NBC

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe.

Manufaa
 • Ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wasambazaji na watu mbalimbali unaofanya nao biashara
 • Unaongeza muda wa kufanya kazi
 • Baadhi ya matawi hufunguliwa hata Jumapili
 • Unakuwa na uwezo wa kujua makusanyo yako kwa kutumia huduma za NBC Online Banking
 • Unapata faida itokanayo na riba kulingana na kiasi cha fedha kinachobaki kwenye akaunti yako kwa siku. Faida hii hulipwa kila mwezi
 • Unaweza kutoa fedha kwenye akaunti yako ya kukusanyia fedha kwa njia ya hundi, hati za malipo au njia yoyote inayokubalika na benki
Taarifa muhimu
 • Inapatikana kwa ajili ya wateja wetu wenye akaunti za kukusanyia fedha
 • Akaunti ya kukusanyia fedha imeunganishwa na huduma za NBC Online Banking ili kukuwezesha kudhibiti fedha zako kikamilifu

Turuhusu tukuletee benki kwenye eneo la biashara yako

Boresha ukusanyaji wa fedha zako na okoa muda wa wateja wako. Tunakuwekea dirisha na mfanyakazi wa benki katika maeneo yako ya biashara na kukusanya fedha kutoka kwa wateja wako kwa niaba yako. Ni njia nzuri na inaokoa muda.

Namna ya kupata Huduma hii

Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe.

Manufaa
 • Inakuongezea ufanisi wa kusanyaji wa fedha
 • Inakupunguzia usimamizi wa ndani
 • Inapunguza mlolongo wa kuhakiki hesabu
 • Inapunguza hatari za usalama
Taarifa muhimu
 • Mfanyakazi wa benki atakupatia risiti za makusanyo yote
 • Tunasafirisha fedha zako na kukuwekea kwenye akaunti yako

Kwa nini kusubiri muda mrefu, wakati tunaweza kukusaidia?

Kitengo chetu cha Huduma ya Kusafirisha Vifurushi inakupatia wakala wa kusafirisha na kukusanya nyaraka zako mbalimbali kama vile hundi, kadi, taarifa na zaidi. Inapatikana wakati wowote na mahali popote.

benefits - icon
Namna ya kupata huduma hii
 • Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe
benefits - icon
Manufaa
 • Inapunguza gharama za uendeshaji
 • Inaokoa muda
 • Ni salama kwani nyaraka zako zitachukuliwa kutoka ofisini na mtoa huduma anayeaminika
benefits - icon
Taarifa muhimu
 • Wakala wetu atakusanya au kukuletea nyaraka kwa wakati wako
 • Wakala wetu anakusanya nyaraka kutoka kwenye eneo la biashara yako na kutuletea Benki
 • Wakala wetu anakusanya nyaraka kutoka Benki na kukuletea kwenye eneo la biashara yako
Professional using a laptop

Shughulikia biashara yako na sisi tutakusaidia kwenye masuala ya kiitifaki

Huduma ya kusafirisha fedha taslimu kwa gari la benki

Mfanyakazi wa NBC anakuja na kuhesabu fedha kwenye eneo la biashara yako, anazisafirisha na kuziweka kwenye akaunti yako. mfanyakazi huyu pia anaweza kutoa fedha kwa niaba yako, kuisafirisha na kuifikisha kwenye eneo lako la biashara.

Huduma ya kusafirisa Fedha taslimu bila gari la benki

Tunakusanya fedha kutoka kwenye eneo la biashara yako na kuifikisha kwa kwenye tawi la NBC ambapo zitahesabiwa na kuwekwa kwenye akaunti yako. Pia tunasafirisha na kukuletea fedha taslimu kwenye eneo lako la biashara na mhudumu wako atazihesabu na kuzipokea.

benefits - icon
Namna ya kupata huduma hii
 • Jaza tu fomu hii nasi tutawasiliana na wewe, au tembelea tawi lolote la NBC lilipo karibu nawe.
benefits - icon
Manufaa
 • Kuchukua fedha taslimu kwa wakati unaofaa kwako
 • Fedha zitawekwa kwenye akaunti yako kwa wakati
 • Unaendelea na biashara yako na kutuachia sisi masuala ya kusimamia fedha yako
 • Unaongeza usalama wa fedha zako
 • Unakuwa salama dhidi ya hatari zinazohusiana na kushughulikia fedha taslimu wakati wa kusafirisha

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191 | 0800711177 (free)

Tuandikie baruapepe:

nbc_businessbanking@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC