Pata fursa ya kupata wateja wengi zaidi na kuuza zaidi kwa kupokea malipo kwa njia ya kadi kwa kutumia mashine za malipo (POS) kwenye eneo lako la mauzo. Ni njia rahisi, nzuri na salama ya kupokea malipo. 

 

card with cash
Punguza Athari

Achana na mzigo wa kutunza fedha taslim kwenye eneo lako la biashara.

Mauzo zaidi

Rahisisha ulipaji na upokeaji malipo kwenye biashara yako na upate vyanzo vipya vya mauzo.

Huduma bila fedha taslimu

Furahia huduma bora na uhuru wa kutumia huduma bila fedha taslimu.

card with cash
Kinga biashara yako

Ikinge biashara yako dhidi ya wizi na uhalifu kwa kufanya miamala isiyohusisha fedha taslimu.

Huduma za ongezeko la thamani

Tunakusaidia kuweka vizuri hesabu za akaunti yako.

Glob icon
Msaada wa kipekee

Pata msaada wa kibiashara kutoka kwenye vituo vyetu vya mawasiliano.

Professional using a laptop

Ongeza thamani ya biashara yako

NBC itakupatia mashine moja ya kupokea malipo ya fedha za Kitanzania na Dola za Kimarekani kwa njia ya kadi. Huduma hii inakusaidia kukidhi mahitaji ya wateja wako.

NBC hutoa mashine zinazopokea malipo zenye GPRS

Oda ya malipo kwa njia ya mashine 

 • Hauhitaji kuwa na kadi (oda inaweza kufanywa kwa njia ya baruapepe kabla mteja hajafika). Kama mteja ataahirisha kuja, fedha zitarejeshwa kupitia mashine hiyo ya malipo au kupitia mfumo wa NBC.

Kulipia kwa kadi kupitia mashine ya malipo

 • Kwa miamala ya kuchanja kadi, mmiliki wa kadi lazima awepo wakati wa kufanya malipo

Tunakupatia mashine inayobebeka, isiyohitaji waya kuunganishwa na huduma nzuri, kama vile:

 • Imeunganishwa kwenye GPRS (makubaliano ya kukupa mtandao wa ziada yanaweza kufanyika)
 • Inatunza chaji kwa saa 3-5
 • Ina uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu
 • Kadi ya chipu yenye uwezo mkubwa
 • Ina kasi kubwa
 • Ina kioo kikubwa cha LCD kwa ajili ya watu kuona vizuri
 • Ni kifaa kidogo kinachobebeka kirahisi (cha kubeba na kisichohitaji waya)

Tunaweza kukupatia mashine nyingi, kutegemeana na ukubwa wa miamala unayofanya. Zaidi ya hayo, tunaweza kukupatia mashine moja inayopokea fedha za kitanzania na za kigeni.

Aina ya kadi zinazoweza kutumika
 • VISA
 • Mastercard
 • China UnionPay International

Tutakupunguzia mzigo wa kutunza fedha taslimu

Tunahudumia wafanyabiashara mbalimbali katika huduma hizi na unaweza kuwa mmoja wao. Panua biashara yako kwa kutumia huduma zetu za kukurahisishia kusimamia fedha zako.

benefits - icon
Tutakupatia mafunzo na Mashine ya malipo BURE

NBC itakupatia mashine ya malipo bure. Pia tutalipia gharama za mtandao za kila mwezi kukuongezea thamani zaidi ya huduma hii. Baada ya kukupa mashine hii, NBC itatoa mafunzo ya kutosha kwako na kwa wafanyakazi wako juu ya namna ya kutumia mashine hii na namna ya kudhibiti uhalifu. Mafunzo mengine yatatolewa pia na NBC kuhusiana na mahitaji na ubereshaji wa huduma hii.

Makato

Utalipia asilimia ndogo kwenye miamala yako yote, na hata hivyo, tunaweza kujadiliana kupadilisha kiwango utakacholipia pale mauzo yanapoongezeka sana.

Kushughulikia Malipo 

Dhamira yetu ni kushughulikia malipo mapema iwezekanavyo na kwa muda mfupi na tunajitahidi iwe hivyo mara zote.

benefits - icon
Kushughulikia matatizo ya miamala na mengine

Malalamiko ya miamala hutokea iwapo mwenye kadi anayo maswali kuhusiana na muamala. Tutajitahidi kushughulikia malamimiko haya na kuhakikisha suluhisho linapatikana haraka iwezekanavyo.

Msaada kwa wateja

Tunajitahidi kuwa na msaada wa saa 16 kila siku kupitia Kituo cha Mawasiliano cha NBC. Pata msaada wa kiufundi na kuzungumza na watoa huduma wetu. Kama mashine inayosumbua haitatengemaa mara moja, suala hili litapelekwa kwa mhandisi mara moja ili kurekebishwa. Lengo letu ni kukupatia huduma za uhakika na kuaminika wakati.

benefits - icon
Huduma nyingine kwa wafanyabiashara 
 • Ina mfumo wa kielektroniki wa kukuwezesha kufunga hesabu
 • Kuna timu maalum inayohusika na usimamizi wa mifumo na masuala yote yanayohusiana na miamala ya kadi
 • Ina taarifa ya kila mwezi ya miamala ya kadi ili kukusaidia kuweka mambo sawa
 • Utapigiwa simu mara kwa mara na kukutembelea kwa ajili ya kutatua changamoto unazokutana nazo na kupata maoni moja kwa moja kutoka kwako

Anza sasa na ukuze bishara yako

Unapoanza, tutakupa fomu ya kujaza na mkataba wa kusaini. Turudishie fomu iliyojazwa na mkataba uliosainiwa.

benefits - icon
Kinachotakiwa kutoka kwako

Tutahitaji nyaraka zifuatazo:

 • Mkataba wa makubaliano
 • Leseni ya biashara
 • Namba ya Mlipa Kodi (TIN)
 • Taarifa ya fedha ya miezi sita ya biashara yako au makadirio ya fedha kama ni biashara mpya
 • Taarifa ya ukaguzi wa hesabu kwa biashara kubwa
 • Mapato ya mwaka ya BRELA (Wakala wa Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara) au hati ya usajili kutoka BRELA
 • Uamuzi wa Bodi uliopitisha kutumika kwa Mashine za malipo kwenye biashara yako
 • Nyaraka za utambulisho wa Bodi ya Wakurugenzi
benefits - icon
Manufaa ya kutumia mashine za malipo:
 • Kupunguza gharama na hatari ya kubeba fedha taslimu
 • Kufungua fursa za mauzo mapya kwa kuongeza aina ya wateja wanaopenda kununua bidhaa na huduma bila kutumia fedha taslimu
benefits - icon
Taarifa muhimu

Fungua Akaunti ya Hundi kwa ajili ya Biashara sasa, ili iweze kutumia huduma hii.

Wateja wetu:

 • Mahoteli
 • Nyumba za kulala wageni
 • Migahawa mikubwa ya chakula
 • Maduka ya jumla na rejareja
 • Mawakala wa usafari
 • Mawakala wa safari za utalii
 • Saluni za warembo
 • Saluni za wanaume
 • Maduka ya madini

Unahitaji maelezo zaidi au msaada?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191 | 0800711177 (free)

Tuandikie baruapepe:

nbc_businessbanking@nbc.co.tz

Wasiliana nasiMatawi ya NBC