Unapata fursa ya kuingia kwenye soko la wateja wakubwa na kuuza zaidi kwa kutumia mashine za POS zinazowekwa kwenye vituo vya mauzo. Ni njia rahisi na nzuri ya kupokea malipo kwa usalama. 

 

card with cash
Punguza hatari

Tua mzigo wa kushughulika na fedha taslimu.

Glob icon
Mauzo zaidi

Ongeza kasi ya kufanya malipo katika vituo vya malipo na fungua vituo vingine vipya ya mauzo.

Huduma zisizotumi fedha taslimu

Furahia uhuru wa kutumia huduma zetu bora zisizotumia fedha taslimu.

card with cash
Kinga ya biashara yako

Ikinge biashara yako dhidi ya wizi na uhalifu kwa kufanya miamala isiyotumia fedha taslimu.

Huduma za ongezeko la thamani

Tunakusaidia kutathmini mwenendo wa akaunti yako.

Glob icon
Msaada wa pekee

Pata msaada wa kibiashara kutoka kwenye vituo vyetu vya mawasiliano.

Professional using a laptop

Ongeza thamani ya biashara ya kampuni yako

Benki ya NBC inakupatia mashine moja ya POS inayopokea fedha za Kitanzania na Dola za Kimarekani. Huduma zetu za mashine za POS zinasaidia kurahisisha malipo kutoka kwa wateja wako.

Benki ya NBC inakupa huduma za Mtandaoni kupitia Mashine za POS

Kuweka nafasi ya malipo kabla ya kufika Mteja

 • Mtoa huduma hahitaji kuwa na kadi ya mteja (yaani kwamfano wa hoteli, mteja anaweza kutuma maombi kwa njia ya baruapepe kabla mteja hajafika). Kama mteja ataahirisha safari na malipo yamefanyika, fedha zitarejeshwa kupitia mashine hiyo ya POS au mfumo wa malipo wa NBC

Kulipia huduma kwa Kadi kwenye Mashine ya POS (kwa kuchanja)

 • Kwa miamala ya kadi kwenye mashine ya POS, mmiliki wa kadi lazima awepo wakati wa muamala

Mashine hizi ni nyepesi na inabebeka kirahisi, haihitaji waya kuunganishwa na zina mambo mazuri, kama vile:

 • Imeunganishwa kwenye GPRS (mtandao wa mawasiliano ya ndani) mazingira huandaliwa kwa ajili ya kuunganishwa upya kwenye mfumo pindi mashine inapo kuwa imeshindwa kuwa hewani
 • Ni ya kuchaji na inatunza umeme kwa saa 3-5
 • Ina uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu
 • Ina cheti cha EMV 4.0 na ina pokea kadi zenye chipu
 • Ina kasi kubwa ya kutuma na kupokea taarifa pindi unafanya miamala
 • Ina kioo kikubwa cha LCD kwa ajili ya watu kuona vizuri
 • Ni kifaa kidogo kinachobebeka kirahisi (cha kubeba na kisichohitaji waya)

Tunaweza kukupatia mashine nyingi, kutegemeana na ukubwa wa miamala unayofanya. Kwa kuongezea, tunaweza kukupatia mashine moja inayopokea fedha za ndani na za kigeni.

Aina ya kadi zinazoweza kutumika
 • VISA
 • Mastercard
 • Kadi za China za UnionPay International

Tutakupunguzia mzigo wa kubeba fedha taslimu

Tunahudumia wafanyabiashara wakubwa katika huduma hizi na unaweza kuwa mmoja wao. Kuza biashara yako kwa kutumia huduma za Wafanyabiashara za NBC.

benefits - icon
Tutakupatia Mashine ya POS na mafunzo bila gharama yoyote

Benki ya NBC itakupatia mashine ya POS bure. Tutakusaidia pia gharama za mtandao za kila mwezi. Baada ya kuamua kuanza kutumia Mashine ya POS, NBC itakupatia mafunzo ya kutosha juu ya namna ya kutumia mashine hii na namna ya kudhibiti uhalifu kwa wafanyakazi wako. Mafunzo mengine yatatolewa pia na Benki ya NBC kuhusiana na taarifa na masharti ya huduma hii.

Kamisheni

Kutakuwa na makato ya asilimia ndogo kwenye miamala yako yote, na hata hivyo, tunaweza kujadiliana kuhusu kiwango hiki pale mauzo yanapoongezeka sana.

Kushughulikia Malipo

Dhamira yetu ni kushughulikia malipo haraka iwezekanavyo. Tena ndio lengo letu na tunadhamiria kulidumisha.

benefits - icon
Kushughulikia fedha zinazorudi na matatizo mengine

Kurudisha fedha ni miongoni mwa matatizo ambayo mwenye kadi anaweza kuwasilisha akilalamikia muamala fulani. Tutajitahidi kushughulikia fedha zinazorudi kwa makini ili kuhakikisha ufumbuzi unapatikana haraka iwezekanavyo.

Msaada kwa wateja

Utapata msaada ndani ya masaa 24 kwa wafanyabiashara kupitia Kituo cha Mawasiliano cha NBC. Pata msaada wa kiufundi na kuzungumza na watoa huduma wetu masaa yote. Kama mashine inayosumbua haitatengemaa mara moja, suala hili litapelekwa kwa mhandisi mara moja. Lengo letu ni kukupatia huduma za kibiashara za kiwango cha juu.

benefits - icon
Manufaa ya huduma kwa wafanyabiashara
 • Ina mfumo wa kielektroniki wa kukusaidia kuhakiki taarifa zako za miamala
 • Kuna timu maalum inayohusika na usimamizi wa mifumo na masuala yote yanayohusiana na miamala ya kadi
 • Ina taarifa ya kila mwezi ya miamala ya kadi ili kukusaidia kuhakiki taarifa zako za miamala
 • Kuwa huru kutupigia simu mara kwa mara na tutakutembelea kwa ajili ya kutatua changamoto zako na kupata maoni yako

Anza sasa na upanue kampuni yako

Unapoanza, tutakupatia fomu na mkataba wakujiunga. Zijaze na kututumia pamoja na mkataba uliosaniwa.

benefits - icon
Mahitaji wakati wa kuanza

Nyaraka zifuatazo utatakiwa kuwa nazo:

 • Mkataba wa makubaliano
 • Leseni ya biashara
 • Namba ya Mlipa Kodi (TIN)
 • Muhtasari wa miezi sita wa biashara yako au dira ya biashara mpya
 • Taarifa ya ukaguzi wa hesabu kwa biashara kubwa
 • Mapato ya mwaka ya BRELA (Wakala wa Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara) au hati ya usajili kutoka BRELA
 • Maamuzi ya Bodi yaliyopitisha kutumika kwa Mashine za POS
 • Nyaraka za utambulisho wa Bodi ya Wakurugenzi
benefits - icon
Manufaa
 • Kupunguza gharama na athari zitokanazo na kubeba fedha taslimu
 • Kufungua fursa za mauzo mapya kwa kuongeza aina ya wateja wanaopenda kununua bidhaa na huduma bila kutumia fedha taslimu
benefits - icon
Taarifa muhimu

Fungua Akaunti ya Hindu ya kampuni sasa ili uwe na sifa ya kupata huduma hizi muhimu.

Wateja wetu:

 • Hoteli
 • Nyumba za kulala wageni
 • Migahawa mikubwa
 • Maduka ya jumla na rejareja
 • Mawakala wa safari za utalii
 • Saluni za warembo
 • Saluni za wanaume
 • Maduka ya Vito

Je, unahitaji taarifa au msaada zaidi?

Tupigie:

+255 768 984 000 | +255 22 219 9793 | +255 768 980 191

Tuandikie Baruapepe:

nbc_corporateservices@nbc.co.tz

Wasiliana nasiTafuta tawi